Historia ya uhasama wa makundi ya hipo hop kutoka East Coast na West Coast!
Ni uhasama uliokuwa gumzo kubwa duniani katika miaka ya 1990's baina ya wasanii na mashabiki wa Hip Hop kutoka kambi mbili za East Coast na West Coast nchini marekani. Inazungumzwa kuwa chanzo kikuu cha uhasama wa pwani hizo mbili ni Rapper kutoka East Coast, Notorious BIG (Akiwa chini ya lebel yake kutoka jiji la New York,Bad bor records), na rapper kutoka West Coast namzungumzia Tupac(Akiwa chini ya lebel yake kutoka jiji la Los Angeles, Death row records), ambao wote walikuja kuuwawa na wauaji bado hawajajulikana. Tupac aliuawa mwaka 1996 na Notorious BIG, mwaka 1997.
Tupac
Notorius B.I.G
Hip Hop kama Hip Hop Kwa ufupi.
Hip hop ilianza katika miaka ya 1970's katika mitaa ya south Bronx. Ikipewa nguvu na Madj kama Dj Herc, Grandmaster flesh na Afrika bambataa. Aina hii ya muziki ilikuja kuwa maarufu katika kila kona ya Bronx.
Maeneo yote ya New York yalibaki kuwa ndio kioo cha music wa Rap katika miaka yote ya 80's ambako ndipo makazi ya mastaa mbalimbali wa Rap kama Run DMC. LL Cool J, KRS One, Dougie Fresh,Rakim,Big Daddy kane, Biz Markie, Slick Rick, Salt N Pepper na wengineo.
Dj Herc.
Grand masterflash
Afrika Bambaataa
Maeneo yote ya New York yalibaki kuwa ndio kioo cha music wa Rap katika miaka yote ya 80's ambako ndipo makazi ya mastaa mbalimbali wa Rap kama Run DMC. LL Cool J, KRS One, Dougie Fresh,Rakim,Big Daddy kane, Biz Markie, Slick Rick, Salt N Pepper na wengineo.
Katika miaka ya mwanzo ya 90's Hip Hop ilifanya kazi kubwa na kuwa sauti ya watu weusi kuongelea matatizo yao kutokana na mtindo au aina ya mashairi yaliyokuwa yakiandikwa. Na kadri muda ulivyozidi kwenda Hip hop na Gangstar rap ziligeuka kuwa kuwa ndio nyenzo za kushindana baina ya Records lebels na makundi ya Kigangstar. Records lebels zilitaka kujenga heshima ili kutaka kufanikiwa kibiashara na kupata biashara kupitia biashara ya music.
Kuibuka kwa West Coast.
Akivutiwa na Rapper kutoka Philadelphia aitwayr Schoolly D, mwaka 1986, Rapper kutokea eneo lijulikanalo kama Crenshaw, Ice T, aliachia wimbo ulioitwa "6 in the morning". Inasemwa na wengi kwamba wimbo huo ndio Gangstar rap song ya kwanza kabisa kwani baada ya wimbo huo ndio Gangstar rap ililipuka na kuchanua.
Ice T
Kijana mmoja Erick wright, ambaye alikuwa akijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya aliona fursa ya faida na umaarufu ya Hip hop. Kwa hiyo alianza kurekodi nyimbo katika studio ndogo iliyokuwa katika garage ya wazazi wake nyumbani kwao.
Erick wright. A.K.A Eazy E
Erick wright ambaye kwa jina la kisanii anajulikana kama Eazy E, aliungana na wasanii wengine Dr.Dre, Ice Cube,Dj Yella na Arabian prince, na kwa pamoja walianzisha kundi lililoitwa N.W.A(Niggers With Attitudes). Kwa msaada wa rafiki yake aliyeitwa Jerry heller, tarehe 3 March 1987, Easy E alianzisha Studio ya kurekodia music iliyoitwa Ruthless Records, na muda mfupi kundi lao liliachia EP iliyoitwa Panic Zone ambayo ilikuwa na nyimbo kama "8 Ball" ya Eazy E na "Dope Man" ya Ice Cube.
Ice Cube
Dj Yella.
Kutokana na kupishana katika masuala ya fedha, Arabian Prince alijitoa N.W.A muda mfupi kabla hawajatoa albamu yao iliyowapa mafanikio makubwa ya "Straight outta Compton", huku nafasi ya Arabian prince ikichukuliwa na Rapper Mc Ren. Albamu hiyo ilibebwa kiasi kikubwa na single "Fuck the Police na "Gangsta Gangsta". Ni albam iliyoitambulisha aina ya music wa hip hop na kusimika rasmi uwepo wa West Coast kwenye dunia ya Rap Music.
Arabian Prince.
Masuala ya fedha yaliua group hili. Eazy E akabaki kuwa mmiliki wa Ruthless Records, Ice cube akawa msanii wa kujitegemea na kuachia albam mbili zilizofanikiwa sana za Amerikkka's most wanted na Death certificate, huku Dr Dre akiungana na Suge knight na kwa pamoja wakawa wamiliki wa Death Row records.
Akiwa Death row records, Dr Dre aliachia albamu ambayo inaaminika ndio albamu iliyoinfluence zaidi Hip Hop duniani iliyoitwa The Chronic. Mastaa wengine waliokuwa chini ya Death row records, walikuwa ni Snoop Dog, Warren G, The lady Rage, Nate Dog, Daz Dillinger na Kurupt waliounda The Dog pound. Hadi kufikia miaka ya 90, West coast ilijipambanua yenyewe kama watawala wa Hip Hop.
Kuibuka kwa East Coast.
Mwezi April 1994, kijana wa miaka 20 kutokea mji wa Qeens, aliyejulikana kama Nassir Jones almaarufu kama NAS, aliachia albamu iliyoitwa Illmatic. Ni albamu iliyokuwa na nyimbo kumi yenye midundo simple na mashairi simple. Kuachiwa kwa albamu hii ilikuwa ni mapinduzi muhimu ya kuirudisha uhai wa East coast, kusaidia kitu kilichoitwa East Coast renaissance.(Kuchipuka upya kwa East Coast.)
Nas
Miezi kadhaa baadaye, Rapper mwingine kutoka New York alirekodi moja ya albamu ya hali ya juu duniani. Naye ni Notorius BIG, akiwa na umri wa miaka 22. Albamu iliitwa Ready to die, na ilipatiwa cheti cha gold ndani ya miezi miwili tu toka iachiwe na kusaidia Bad boy records kuonekana kwenye ramani, ikifuatia mafanikio ya albamu ya Craig mack, "Flava in ya ear", na pia kufuatia mafanikio ya The Wu Tang Clan.
1:Bad Boy Records VS Death Row Records.
Mwaka 1993, Puffy Daddy alianzisha Hip Hop lebel iliyokuwa New York, ikijulikana kama Bad Boy Records. Mwaka uliofuatia yaani 1994, Bad Boy Records iliachia alnabu mbili kutoka kwa Notorius BIG na rapper kutoka Long Island aliyeitwa Craig Mack, albamu ambazo zilifanikiwa sana kibiashara.
Ghafla aliibuka rapper mmoja kutoka California aliyeitwa Tupac Shakur alidai kuwa kulitokea tukio la uporaji na yeye alipigwa risasi 5 akiwa Quad Recording studios huko mjini Manhattan, tarehe 30 Novemba 1994, na hadharani alidai kuwa waliohusika katika tukio hilo ni Notorius BIG, Andre Harrell na Puffy Daddy.
Siku chache baada tukio hilo la kupigwa risasi Tupac na tuhuma alizozitoa, single iliyoitwa "Who shot ya" kutoka kwa Notorius BIG ilitoka hewani na kuleta hisia kwamba single hiyo ililenga kumjibu Tupac kutokana na tuhuma alizotoa ingawa Puffy Daddy na Notorius BIG walipinga wakisema single hiyo ilikuwa imesharekodiwa kabla hata ya tukio la kupigwa risasi Tupac.
Mwezi August 1995, Suge knight, bosi wa Death row records aliongea maneno haya akiwa anahutubia kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za Source.(Source Awards). "Any artist out there that want to be an artist and stay a star, and don't have to worry about the executive producer trying to be all in the videos...all the records...dancing,come to death row." (Akimaanisha msanii yeyote ambaye anataka kuwa msanii na kubaki kuwa staa, ambaye hatohofia bosi wa lebel yake kujaribu kutokea katika video zake zote, kutokea katika nyimbo zake zote akicheza, basi anatakiwa ahamie Death row.) Maneno hayo moja kwa moja yalionekana kumlenga Puffy Daddy kwani ni kweli ana tabia hiyo ya kutokea katika video za wasanii walio chini yake hata kama hajaimba kitu huku akicheza. Ni dongo ambalo sio tu lilimlenga Puffy daddy bali lilichukuliwa kama tusi kwa wasanii wote wa Hip hop wa East coast.
Siku hiyo hiyo baadaye, uhasama ulizidi kutanuka kati ya East Coast na West Coast wakati Suge knight alipohudhuria party moja iliyoandaliwa na Jermine Dupri huko Atlanta. Wakati Party ikiendelea, rafiki wa karibu wa Suge knight aliyeitwa Jake Robles alipigwa risasi hapo hapo kwenye party. Suge knight bila kupepesa macho alimtuhumu moja kwa moja Puffy daddy ambaye naye alikuwemo kwenye party hiyo kuwa kwa namna moja au nyingine alihusika katika ufyatuaji risasi huo.
Puffy Daddy
Mwaka huo huo Tupac alitupwa jela kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia na Suge knight alikwenda kumdhamini kwa kiasi cha dola 1.4 milioni ili aachiwe kutoka jela kwa makubaliano kuwa akiachiwa tu basi asaini mkataba wa kuwa chini ya Death Row Records. Baada ya Tupac kuachiwa kweli alitimiza makubaliano hayo kwa kusaini mkataba jambo lililozidisha uhasama kati ya Death Row Records na Bad Boy Records kwani tayari Tupac alikuwa na uhasama na Puffy dady na Notorius BIG kwa kuwatuhumu walimpiga risasi 5 kwenye tukiola uporaji huko Quad recording studios, Manhattan, tarehe 30 Novemba 1994.
2:Tupac VS Notorius BIG.
Kwenye wimbo wa Notorius wa "Who shot ya", kuna mstari unasema, "Come here..come here...open your fucking mouth...Didn't I tell you not to fuck with me?...cant talk with a gun in your mouth huh? Bitch ass nigga,what.(Kwa kifupi ilitafsiriwa kwamba alikuwa akimuimbia Tupac kuhusu tukio la kupigwa risasi kwake.)
Notorious B.I.G
Katika wimbo wa Tupac, "Hit em up", kuna mstari unasema, "who shot me, but punks didn't finish now you are about to feel the wrath of a manace nigga. I hit em up!"(Unaweza ukaona ni mistari ilikaa wazi kama jibu la moja kwa moja kwa nyimbo ya "who shot ya".)
Miaka ya mwishoni 1995 mpaka mwanzoni 1996 Tupac alitoa mfululizo wa nyimbo nyingi zikimlenga kumtukana, kumtishia na kumdhalilisha Notorious BIG, Bad boy records na wasanii wote waliokuwa chini ya lebel hiyo. Mfano nyimbo kama "Against all odds", "Bomb first" na "Hit em up".
Tupac
Notorious BIG naye hakuwa nyuma kwani aliachia nyimbo iliyoitwa, "Long kiss goodnight" ambayo mashairi yake yalionekana kumlenga Tupac na hata memba mmoja wa Bad Boy Records aitwaye Lil cease akihojiwa na XXL magazine alikiri kuwa nyimbo hiyo ilimlenga Tupac ingawa bosi wa Bad boy, puffy daddy, alikanusha mara moja akisema nyimbo hiyo haikumlenga Tupac, na kudai kama Notorious akitaka kumuimba Tupac basi atamtaja kwa jina moja kwa moja sio kuuma maneno.
Katika kipindi hicho vyombo vya habari viliripoti sana matukio haya na kwa kiasi kikubwa vilishiriki kuzidi kuchochea uhasama zaidi baina ya pande hizo mbili na hivyo kusababisha sasa hadi mtaani mashabiki kujitenga kwa kuchagua upande wa kushabikia hivyo uhasama ukahamia pia kwa mashabiki.
Tarehe 13 Septemba 1996, Tupac alifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa kwenye gari siku sita nyuma, alipokuwa akitoka kuangalia pambano la ngumi la Mike Tyson, huko Las Vegas, Nevada.
Mwandishi mmoja aitwaye Chuck Philips aliandika kwenye makala moja iliyokuwa na kichwa cha habari,"Who killed Tupac Shakur", kuwa shambulio hilo lilifanywa na kundi moja la kihuni la Compton lijulikanalo kama South side crips, kulipiza kisasi cha mwenzao mmoja ambaye alipigwa na Tupac masaa kadhaa nyumba kabla ya shambulio hilo. Memba huyo aliyejulikana kama Orlando Anderson alikamatwa na polisi wa Las vegas na kuhojiwa mara moja tu kabla ya kuachiwa huru. Siku chache tu baada ya kuachiwa huru, Orlando Anderson aliuawa kwa risasi katika mapigano ya makundi mawili ya kihuni.(Inahisiwa hilo kundi jingine likuwa supporters wa Tupac, ni kama walienda kulipa kisasi na wao).
Chuck Phillips
Orlando Anderson
Miezi sita baada ya kifo cha Tupac, tarehe 9 Machi 1997, Notorious BIG naye aliuawa kwa risasi huku muuaji akiwa hajulikani huko Los angeles. Mpaka leo hii mauaji hayo yamebaki kuwa hayajulikani kuwa yamefanywa na nani, ingawa wengi wanaamini Suge knight anahusika kutokana na mlolongo wa matukio ulivyo.
Baada ya vifo hivyo, uhasama nao ukaoungua kwa kiasi kikubwa kama sio kwisha kabisa.