LOGO

LOGO

Thursday 18 June 2015

Watu maarufu duniani waliojifungua watoto baada ya kufikisha umri wa miaka 40 na zaidi!

Imekuwa ni kama si jambo la kawaida sana kuona mwanamke ameshika ujauzito akiwa na umri mkubwa, kwa mfano kuanzia miaka arobaini. Hii inasababishwa na sababu mbalimbali lakini sababu kubwa zikitajwa kuwa ni za kiafya zaidi kwani mara zote wataalamu wa afya au madaktari wamekuwa wakitahadharisha kuwa uzazi katika umri mkubwa si salama sana na mara nyingi hushauri kama umri umeshakutupa mkono basi jitahidi usishike ujauzito. Lakini hapa ninakuletea list ya watu maarufu duniani ambao wao hawakulizingatia hilo na walishika ujauzito na kufanikiwa kupata watoto. 

1.Gwen Stefan.
Gwen Stefan alikuwa ana miaka 44 wakati anajifungua motto wake anayeitwa Apollo Bowie Flyinn, kujumuika na watangulizi wengine wa kiume aliowapata katika umri wa 30's ambao ni Kingston na Zuma.

2.Rachel Zoe.
Rachel Zoe alikuwa ana miaka 42 wakati anatangaza kwamba anategemea mtoto wa pili pamoja na mumewe Rodger Berman.

.3.Halle Berry
Super diva Halle berry alikuwa ana miaka 41 alipopata mtoto wake wa kwanza binti aitwaye Nahla Ariela Aubry, mwezi Machi 2008. Kutokana na maneno yasemwayo kuhusu ujauzito katika umri mkubwa, Halle berry alisema,"Mimba yangu ilikuwa ya ajabu sana. Nilikuwa nina furaha muda wote, nilikuwa najisikia vyema muda wote, nilikuwa nina nguvu. Nilikuwa kama superwoman. Natamani ningekuwa najisikia kama vile katika maisha yangu yote." Na kwa kuthibitisha maneno yake hayo, Halle berry alipata mtoto wa pili aitwaye Maceo wakati akiwa na umri wa miaka 47.

4.Kelly Preston.
Baada ya kumpoteza mtoto wao wa kiume,Tett, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 16, Kelly Preston na mumewe John Travolta waligubikwa upya na furaha wakati Kelly Preston alipojifungua bila matatizo yoyote mtoto wa kiume waliyempa jina la Benjamin, mwaka 2010, akiwa katika umri wa miaka 48.
Akiongea na kipindi cha televisheni cha Today show muda mfupi baada ya kujifungua kutokana na hatari ya kujifungua katika umri mkubwa alisema,"Sikuangalia kabisa kuhusu hatari iliyopo, pekee nilichofikiria ni ugumu utakaokuwepo wakati wa kujifungua."

5.Marcia Gay Harden.
Marcia gay harden alikuwa na miaka 44 wakati anajifungua mapacha wake, Hudson na Julitta Dee, katika ndoa yake na mumewe Thaddaeus Scheel. Lakini pamoja na ujauzito huo tayari alikuwa na binti mwingine, Eulala Grace, aliyempata akiwa na umri wa miaka 41.

6.Tina Fey.
Ni mwanadada muigizaji ambaye alipata mtoto wa pili aitwaye Penelope akiwa na umri wa miaka 41, akimfuatia wa kwanza aliyeitwa Alice.

7.Salma Hayek.
Muigizaji nyota Salma Hayek alikuwa na umri wa miaka 40 wakati alipojifungua binti yake aliyekuja kupewa jina la Valentina paloma pinault, kutoka katika ndoa yake na mumewe Francois-Henre Pinault.

8.Susan Sarandon.
Susan Sarandon alipata mtoto wake wa kwanza ambaye ni wa kike aitwaye Eva Amurri katika umri wa miaka 39. Bila watu kutarajia alipata mtoto wa pili ambaye ni wa kiume aitwaye Jack Henry, akiwa na umri wa miaka 42.Wakati watu wakidhani umri sasa umeshamtupa mkono, aliwastua kwa kuwaletea mtoto wa tatu ambaye alikuwa ni wa kiume pia aitwaye Miles Guthrie wakati alipofikisha umri wa miaka 45.

9.Kim Basinger.
Kim basinger akiwa kwenye mapenzi motomoto na mcheza sinema Alec Baldwin, walifanikiwa kupata mtoto wa kike wakati Kim Basinger akiwa na umri wa miaka 41.,

10.Brooke shields.
Brooke shields alipata mtoto wake wa kwanza binti anayeitwa Rowan Francis mwaka 2003 wakati huo akiwa na umri wa miaka 38. Miaka mitatu baadaye yaani mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 41, alimkaribisha duniani binti mwingine aliyempa jina la Grier.

11.Celine Dion.
Baada ya kusumbuliwa sana na masuala ya uzazi hususani kutoka kwa mimba mara kadhaa (Miscarriage), hatimaye Celine dion alipewa zawadi ya kipekee na mwenyezi Mungu kwa kujifungua watoto mapacha, Eddy na Nelson, akiwa na umri wa miaka 42 pamoja na mumewe Rene' Ange'lil.

12.Molly Ringwald.
Molly Ringwald alikuwa na miaka 41 wakati alipopata ujauzito na kujifungua watoto mapacha,Roman Stylianos na Adele Georgiana, mwaka 2009. Lakini tayari alikuwa mama wa binti aitwaye Mathilda Ereni.

13.Hellen Hunt.
Kellen Hunt alikuwa na miaka 40 wakati akijifungua binti yake aliyempa jina la Makena Lei Gordon Carnahan.

14.Geena Davis.
 
Geena Davis mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 46, alipata mtoto aitwaye Alizeh. Watu walimshangaa kuzaa katika umri wa miaka 46 lakini yeye akaamua kuwakomesha watu hao kwani mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 48 alijifungua tena watoto mapacha,Kian na Kaiis.

15.Meryl Streep.
Meryl streep alipata mtoto wake wa nne aitwaye Louisa Jacobson Gummer mwaka 1991 muda mfupi kabla hajatimiza umri wa miaka 42.

16.Nicole Kidman.
Nicole Kidman tayari alikuwa mama wa watoto wawili, Isabella na Conor, watoto waliowaasili yeye pamoja na mpenzi wake wa zamani Tom cruise. Lakini alikuja kupata mtoto wake wa kumzaa mwenyewe mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 40.

17.Mariah carey.
Mariah carey alipata watoto akiwa na umri wa miaka 42, mwaka 2011. Watoto mapacha,Moroccan na Monroe. Naye hapo awali alikuwa na tatizo la mimba kutoka(Miscarriage), kwa hiyo kupata mapacha hao ilikuwa Baraka kubwa kwake.

18.Marcia cross.
Katika kipindi cha ndani ya mwaka mmoja, Marcia cross alipata neema mbili kwa pamoja. Kwani alifunga ndoa mwaka 2006 na Tom Mahoney na pia February 2007 alipata watoto mapacha, Eden na Savannah, muda mfupi kabla hajatimiza umri wa miaka 45.

19.Beverly D'angelo.
Mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 49, Beverly D'angelo alijifungua watoto mapacha, Anton na Olivia Pacino, baba akiwa na star wa movie aitwaye Al Pacino.

20.Mira Sorvino.
Baada ya mimba iliyomsumbua sana, hatimaye Mira sorvino alijifungua mtoto wake wa tatu, Holden Paul Terry, mwezi June, mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 41.Hakukoma! Mwezi May, mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 44 alipata mtoto wake wa nne, binti Lucia. Mira Sorvino na mumewe Chris Backus tayari awali walikuwa wana watoto wawili, Johnny Christopher King na Mattea angel.

21.Cheryl Tiegs.
Cheryl Tiegs alipata mtoto wake wa kwanza, Zack, akiwa na umri wa miaka 44 kutoka kwenye ndoa na mumewe wa zamani Antony peck. Akawaacha watu midomo wazi mwaka 2000 kwa kupata mapacha na mumewe Rod Stryker, mapacha Jaden na Theo, akiwa na umri wa miaka 52!

22.Jennifer connely.
Jennifer connely alikuwa na umri wa miaka 40 wakati yeye na mume wake Paul bettany walipoongeza mtoto wa tatu Agnes lark, kuungana na kaka zake waliomtangulia, Kai na Stellan.Hiyo ilikuwa ni May 2011.

23.Mary Stuart Masterson.
Mary stuart masterson alifanya kweli kwa kupata mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 43, na mumewe wa  tatu, Jeremy Davidson. August 2011 walikaribisha watoto mapacha Mary Stuart Masterson akiwa na miaka 44. Kuonyesha uzazi wake aliupanga kila baada ya mwaka mmoja, October 2012, akiwa na umri wa miaka 45, akapata mtoto wa nne.

24.Uma Thurman.
Baada ya kupata watoto wawili na mume wake wa zamani Ethan hawke, ambao ni Maya na Leven, Uma Thurman alimkaribisha mwanaye wa tatu Rosalinda Arusha ArkadinaAhalune Florence Thurman-Busson, mwezi July 2012 akiwa na umri wa miaka 42.

25.Julianne moore.
Mwezi April 2002, Juliane moore alipata mtoto wake wa pili,Liv, akiwa na umri wa miaka 41. Mtoto wake wa kwanza anaitwa Caleb.

26.Naomi watts.
Naomi watts alianza kutengeneza familia yake mwaka 2007, baada ya kuzaliwa kwa mtoto Sasha wakati huo akiwa na miaka 39. Mwaka mmoja baadaye yaani December 2008, akiwa na umri wa miaka 40, aliimarisha familia yake kwa kujifungua mtoto wa kiume anayeitwa Samuel. 

No comments:

Post a Comment