LOGO

LOGO

Tuesday 16 June 2015

Visingizio Baada ya timu kufungwa!!

Visingizio vya kijinga zaidi kutoka kwa makocha na wachezaji!

Katika soka waandishi wa habari wanakutana na visingizio vingi kutoka kwa wachezaji na makocha wa timu mbalimbali kutokana na matukio mbalimbali ya ndani na nje ya uwanja.Hata hivyo, kuna visingizio vingine vinachekesha sana.

1.Kutoka kwa Francesco Totti na Christian Panucci.
Francesco totti.

Christian Panucci.

Mfanyakazi mbovu kila siku atalaumu zana zake. Na ndicho kilichotokea kwa mastaa wawili wa timu ya taifa ya Italia, Francesco Totti na Christian Panucci baada ya suluhu ya 0-0 dhidi ya Denmark michuano ya Euro 2004.
Totti aliamua kulaumu vikali kuhusu viatu vyake huku akidai kwamba kuvaa viatu hivyo ilikuwa ni sawa na kutumbukiza mguu wako katika mchanga unaochemka. Panucci ndiye aliyetoa kali zaidi kwa kulaumu soksi zake."Nyuzi ambazo zimetumika katika kutengeneza soksi hizi zimetengenezwa vibaya sana."
Kweli wachezaji wa kulipwa kama hawa wanaweza kutoa visingizio hivi kweli eti kuwa ndio sababu ya kutoka suluhu?

2:Kenny Dalglish.
  
Mara nyingi makocha mbalimbali duniani huwa wanalia sana na waamuzi pindi matokeo yanapokuwa yale ambayo hawayajayatarajia.Lakini wapo makocha wengine ambao huwa wanalia na uzembe wa wachezaji wao katika kutimiza majukumu yao.
Hata hivyo mwaka 1998, kocha wa New castle united, Kenny Dalglish alikuja na kisingizio tofauti kabisa ambacho hakikutegemewa na yeyote yule wakati New castle iliposhindwa kuifunga timu isiyo katika daraja lolote lile ya Stevenage Borough katika michuano ya kombe la FA. Daglish alilalamika mipira iliyokuwa inatumika katika mchezo ule ilikuwa inadunda sana, eti ndio maana wakashindwa kuifunga timu ile.

3.Yaya Toure.
 
Baada ya kumalizika kwa michuano mbalimbali msimu wa 2013-14, kiungo wa Manchester city, Yaya Toure alitoa madai ya kushangaza na ya kitoto kuwahi kutolewa na mchezaji wa aina yake.
Toure kupitia wakala wake, Dimitri seluk, alidai kwamba alikuwa anafikiria kuondoka Manchester city kwa sababu timu hiyo ilikuwa haimpendi na ilishindwa hata kumpelekea keki maalumu katika sherehe yake ya kuzaliwa alipotimiza miaka 31, Mei 13,2014.
Hivi ni kweli klabu inayokulipa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki unaweza kusema inakupuuza kwa sababu tu ya kushindwa kukuletea keki?

4.Sir Alex ferguson.
Bingwa mwingine wa visingizio huyu hapa. Kwa miaka mingi ya utawala wake old traford, sir Alex erguson alikuwa analaumu vitu mbalimbali kama Manchester united ikichemsha.
Hata hivyo mwaka 1996, wakati Manchester united ilipopigwa bao nyingi na Southampton, Ferguson alikuja na kisingizio cha kuchekesha kweli kweli.
Ferguson alidai kwamba timu yake ilipoteza mechi hiyo kwa sababu ilikuwa imevaa jezi za kijivu. Akadai kwamba wachezaji wake walikuwa hawaonani vizuri uwanjani kutokana na rangi za jezi hizo.
Hata hivyo kisingizio cha Ferguson kilionekana cha uongo zaidi kwani walibadili jezi wakati wa mapumziko na bado ikafungwa mabao matatu zaidi kipindi cha pili.

5.Wayne rooney.
Yaya toure si mchezaji wa kwanza kuishawishi klabu yake kumpa mkataba mpya kwa kutumia sababu za kitoto.
Mwaka 2010, staa wa Manchester united, Wayne rooney aliripotiwa akida kwamba alikuwa anataka kuondoka klabuni hapo kwa sababu ya klabu hiyo imekosa tama ya mafanikio.
Hata hivyo, wiki moja baadaye Rooney aliongezewa mshahara wake kufikia pauni 250,000 na kelele zake zikaisha.

6.Vladislav vashchuck.
 
Katika fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini ujerumani, Ukraine ilichapwa mabao 4-0 na Hispania. Wakati ikionekana kuwa labda waukraine wangeweza kukubali kichapo hicho na kukiri kwamba walikuwa wamezidiwa,kumbe beki wao,Vladislav vashchuck alikuwa na mawazo mengine kabisa.

Vashchuck alilaumu kelele za vyura waliokuwa wanalia nje ya ya hoteli waliyofikia usiku wa kuamkia siku ya mechi kwa madai waliwakosesha usingizi na hivyo kuwafanya wawe wachovu siku ya mechi.
"Kwa sababu ya vyura kupiga kelele hatukuweza kupata walau lepe la usingizi.Wote tulikubaliana tuchukue fimbo kwenda nje kuwawinda na kuwapiga." Alisema Vashchuck.

7.Jose Mourinho.
 
Orodha hii ya visigizio haiwezi kukamilishwa bila ya kuwepo kocha huyu wa kireno mwenye maneno mengi.Ni mtaalamu wa visingizio.
Mwaka 2011 alipoteza pambano la supercopa dhidi ya Barcelona iliyokuwa katika ubora wa hali ya juu sana, haikutazamiwa kuwa Mourinho aliyekuwa kocha wa Real Madrid angewapongeza Barcelona kwa sababu ni kocha mwenye majivuno mengi, lakini hata hivyo kisingizio alichotoa kilichosha wengi.
Mourinho alilalamika kwamba katika pambano hilo hakukuwa na watoto waokota mipira inapotoka nje wa kufanya kazi hiyo kwa haraka."Hakukuwa na watoto waokota mipira katika kipindi cha pili." Alilalamika Mourinho, eti ndio sababu ya wao kufungwa pambano lile.

8.Kolo Toure.
Inaonekana familia ya kina Toure ina vichekesho vya kushangaza, baada ya kufungiwa miezi sita kutokana na kufeli katika vipimo vya dawa za kuongeza nguvu, Kolo aliamua kupeleka kesi hii kwa mkewe.
Alidai kwamba dawa hizo alipewa na mkewe kwa ajili ya kupunguza uzito lakini kumbe zilikuwa na chembe chembe za dawa za kuongeza nguvu.Alitoa kauli hiyo utafikir si mchezaji wa kulipwa.

9.Crystal palace.
 
Mashabiki wa mpira ni hodari sana wa kukosoa timu zao pindi zinapofanya vibaya. Hata hivyo mnamo mwaka 2011,mashabiki wa klabu ya crystal palace, baada ya timu yao kufanya vibaya waligundua kwamba sababu  kubwa haikuwa wachezaji.
Mashabiki wa palace waliamua kuwa ni mashabiki warembo wanaoikaribisha timu hiyo uwanjani wakati wa kuingia maarufu kama cheerleaders ndio waliokuwa sababu ya timu kufungwa kwa sababu wachezaji walijikuta wakiwakodolea macho zaidi kuliko kuzingatia soka.
Shabiki mmoja alikwenda mbali kwa kusema,"wanamuondoa kila mtu mchezoni.Unaona wachezaji wanavyowaangalia wao tu wakati ambapo inabidi wazingatie mechi.Afadhali warembo hao waondolewe"

10.Adrian Bradbnam.
Moja kati ya visingizio vya kipumbavu katika soka kimojawapo ni hiki cha mshambuliaji wa wa klabu ya Sutton united, Adrian bradnam, ambaye aliwahi kulaumiwa kwa kukosa bao la wazi kabisa akitizamana na nyavu.
Bradnam alijibu mapigo kwa kudai alikosa bao hilo kutokana na kelele nyingi za mashabiki uwanjani hapo. Hivi mchezaji wa kulipwa unategemea nini ukienda katika uwanja wa soka na katika pambano la ushindani?

Visingizio tu, noooma saaaana!!
Kwa hisani ya gazeti la mwanaspoti.

No comments:

Post a Comment