LOGO

LOGO

Wednesday 21 October 2015

Flaviana Matata...Matata kama jina lake!

Flaviana matata ni mrembo wa kitanzania, aliyezaliwa tarehe 09 June 1988, mkoani Shinyanga nchini Tanzania. Ni mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu huko Arusha akichukua masomo ya electrical engineering kabla ya kuitupa chini fani hiyo na kujikita kwenye fani ya urembo akijishughulisha zaidi na kazi ya modelling, akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 9, nywele nyeusi na macho ya brown.
Safari yake ya mafanikio katika modelling ilianza pale aliposhiriki shindano la kwanza kabisa la miss universe  Tanzania mwaka 2007 na kuwa mshindi wa kwanza hivyo kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika shindano la dunia la miss universe mwaka huo huo wa 2007. Huko alishiriki na alifanikiwa kuingia katika kundi la mwisho la washiriki 15 (Top 15 semifinalist). Na hapo ndipo milango ilipofunguka kwa kujulikana zaidi Tanzania, afrika na duniani kwa ujumla na ukawa ndio mwanzo wa deals mbalimbali kumuangukia.
Alifanikiwa kufanya tangazo la kuchapisha la modelling kwa ajili sherri hill. Na mwaka 2011 alishinda taji taji la model of the year wa jarida la Arise magazine katika Lagos fashion week. Pia ametokea katika magazine mbalimbali maarufu duniani  kama Dazed&comfused, Glass magazine, L'official na i-Dmagazine.

Amefanya pia catwalk kwa ajili ya brands za wabunifu maarufu kama mustafa hassanali, Vivienne westwood, Tory burch suno na Loiise gray.

Mwenyewe akijielezea alipohojiwa na mtandao mmoja anasema, "mimi ni fundi umeme kama kitu nilichosomea, lakini pia ni Top model nchini mwangu. Naamini kwamba mungu ameniumba kiusahihi na asilia haswa, na ni mwanamke asilia wa kiafrika." Na kweli hakuna wa kupingana na kauli yake, Flaviana matata ni mwafrika haswa kwa mwonekano. Asilia na halisi!!

Mama yake alifariki kwa ajali ya Mv Bukoba katika ziwa Victoria nchini Tanzania, wakati huo Flaviana matata akiwa na umri wa miaka 9  tu.

Kifo hicho ndicho kilichomsukuma mwaka 2011 kuanzisha Flaviana matata Foundation kama kumbukumbu kwa mama yake, mfuko unaojishughulisha na elimu na maendeleo ya mtoto wa kike nchini Tanzania.
Akiizungumzia Tanzania anasema, nafikiri Lushoto, huko kwenye milima ya usambara ni siri iliyojificha ukizungumzia utalii wa Tanzania. Ni sehemu iliyo juu ya milima, ni mji uliotengenezwa na wakoloni wa kijerumani na ni kama Uswisi ukizungumzia muonekane wake. Hali ya hewa imepoa."


Flaviana matata ameolewa na kijana mmoja mtanashati anayeitwa Deo Massawe!



No comments:

Post a Comment