LOGO

LOGO

Friday 23 October 2015

Linaitwa "The heat."

Kwa wale walio na pesa ya kuchezea hususani wapenda kusafiri popote pale duniani, basi nalileta kwenu nyumba ya kifahari itembeayo.(Luxury mobile home).

Ni basi liitwalo 'The heat', ambalo ndani yake lina kila kitu kinachotakiwa kuwepo kwenye nyumba yoyote iliyokamilika na kujitosheleza.

Ni basi la ghorofa mbili ambalo kama utahitaji kwa ajili ya kulikodi kwa ajili ya safari zako mbalimbali aidha za utalii au kula raha tu huku ukizunguka maeneo mbalimbali, basi linapatikana kupitia kampini ya Anderson mobile estates, ni mkwanja wako tu!!

Ni basi lenye masterbedroom, vyumba kadhaa vya wageni, mabafu kadhaa na jiko lililokamilika kwa kila kitu.

Kama mpenzi wa kusafiri kwa nini uhangaike kutafuta vyumba vya hoteli, wakati unaweza tu kuishi kwenye hoteli inayotembea muda wowote utakaotaka wewe?


Inaweza ikawa gharama kubwa, lakini itakufanya ujisikie huru huku ukijua kuwa muda wowote ni just kuweka switch on tu na kwenda mahala pengine!!!

No comments:

Post a Comment