LOGO

LOGO

Wednesday 11 November 2015

Ideas za kupiga picha!!

Gobe Mc Clintock ni mpiga picha raia kutoka Canada katika mji wa Calgary ambaye anafanya mfululizo wa picha za kustua za harusi huko Iceland.
 
Akiwa amelipwa na Sarh na Josh, ambao walikuwa wamepanga kufanya sherehe ndogo tu ya harusi pamoja na familia zao na rafiki zao wa karibu huko Ohio, lakini Gabe Mc clintock yeye aliwafanyia kitu tofauti kwa kwenda kuwapiga picha za harusi sehemu tofauti kabisa na zilizozoeleka.
 
Iceland inajulikana kwa landscape yake ya asili iliyo tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani, kwa hiyo haikushangaza hali hiyo kumfanya Gabe Mc clintock kuitumia ipasavyo sehemu hiyo kwa matukio ya picha.
 
Kwa uamuzi huo Sarah na Josh walisema, "ndio, marafiki zetu ni wa kuvutia na wamefanya mambo mengi mazuri kwenye maisha yetu, lakini harusi ilikuwa ni yetu kuifanya na kuitunza mioyoni mwetu. Tukaamua kwamba kama tukitumia pesa nyingi kwa ajili ya harusi yetu, basi hiyo itumike zaidi kwenye kumbukumbu yao." Na ndio maana wakaamua kuteketeza pesa kutoka Ohio kwenda Iceland kwa ajili tu ya kwenda kupiga picha milimani, kwa ajili ya kumbukumbu ya harusi yao!!!!

No comments:

Post a Comment