LOGO

LOGO

Wednesday 4 June 2014

Dunia inaelekea mwisho


Kanisa la White Tail Chapel linakukaribisha kwenda kusali lakini ukiwa uchi wa mnyama!

White tail chapel ni kanisa linalopatikana kwenye viwanja vya white tail resorts huko Ivor, Virginia nchini marekani. Ni kanisa la ajabu kabisa ambalo linaalika watu kwenda kusali na kuabudu mungu wakiwa uchi wa mnyama kabisa, hauruhusiwi kuvaa hata kipande cha nguo.


Muhubiri akiwa madhabahuni, akitoa neno la mungu.

Wenyewe wanasema unaalikwa kusali na kuabudu huku ukifurahia uasili wako wa mungu alivyokuumba, wakiwa na maana mungu hakutuumba tukiwa na tumevaa nguo sasa kwa nini tumuombe na kumuabudu tukiwa na nguo?



Imani yao inawatuma zaidi kwamba, kusali uchi ni kunaleta usawa mkubwa na kuondoa uwezekano wa kuanza kumkagua muumini mwenzako kwa jinsi alivyovaa au nafasi yake katika jamii.



Ingawa ni kweli kwamba siku hizi nyumba za ibada hususani makanisani kumekuwa na tabia za watu kuangaliana nani kavaa zaidi. Wao kwa kuliona hili wakaona dawa ni kuabudu uchi ili akili yote ibaki kwenye ibada na sio kuangalia dada yule kavaa gauni gani au kaka yule ile suti kainunua wapi na mimi nikaitafute.

Sawa lakini mmh........uchi!? Haya kila mtu na imani yake!!

No comments:

Post a Comment