LOGO

LOGO

Friday 15 August 2014

Idea za kushangaza zitakazofanya nyumba yako ionekane tofauti!

Wanasema kipenda roho hula nyama mbichi. Kila mtu anapenda kitu anavyopenda kiwe. Leo tuangalie dizaini mbalimbali za jinsi watu walivyoamua nyumba zao zionekane tofauti kwa jinsi tu walivyopenda wao.
 Aquarium Bed..... Yaani kitanda kinakuwa na sehemu ya kufugia samaki.

 Chandelier that turns your room into a forest.......Ni aina fulani ya taa ukiwasha tu chumba kinakuwa kama msitu.

 Indoor - outdoor pool..............Bwawa la kuogelea linaanzia ndani mpaka nje. Unaamua tu leo uogelee ndani au ukaogelee nje.

 Swing set table...................Ni kama bembea. Tumezoea kuona bembea nje lakini kwa aina hii ni sebuleni, unapata chai huku unaswing.

 Spiral staircase slide..............Ngazi za kuzunguka lakini pembeni yake inazungukwa na sehemu ya kuslide. Kazi kwako kama unaona uvivu kushuka na ngazi basi unaslide tu mpaka chini. Watoto sasa ndio watapata pa kuchezea!


 Cat transit system...............kwa wale wapenda paka lakini hawapendi uchafu. unaweza ukaweka mfumo huu wa kumfanya paka ajivinjari huku na kule lakini kwa njia maalumu.

 Glass floor.........


 Fusion dining table................Ni dining table ambayo baada ya kumaliza mambo ya maankuli unaweza ukaifungua na ikawa pool table.

 Hammock bed.....................Raha jipe mwenyewe kitanda cha kunin'ginia.

 Understairs storage..........Hii safi sana, badala ya nafasi ya chini ya ngazi kukaa bure jamaa wakafanya utundu ikapatikana droo za kuwekea vitu hata nguo.

 Backyard cinema................mambo ya kufunga mini cinema garden.


 Ping pong door............NI Mlango lakini pia unaweza ukawa sehemu ya kuchezea tennis

 A wall that plays music when it rains..........Mabomba yametengenezwa kwa namna ya trumphets mvua ikinyesha maji yakipita ndani yanatoa milio tofauti kiasi cha kuleta ladha tamu ya music.


 Herb garden in your kitchen...............


 Bookcase staircase..................ni yale yale matumizi bora ya ngazi. Pembeni pamefanywa kama shelf ya vitabu.

 Backyard beach............kwa wenye maeneo yao unaweza nyuma ya nyumba yako ukaweka beach yako kama hii.


 Spiral wine storage.....................Ni sehemu ya kuhifadhia wine amnayo ipo chini ya ardhi. Unafungua tu kioo cha juu unakutana na ngazi unaenda kuchagua wine yako.



 Hammock over the stairs...........Kama huna uwezo wa kujenga ghorofa na una hamu ya kuwa unapanda ngazi kwenda kulala juu, basi fanya hivi.

 Walk in pool...........Tumezoea kuona pool za kushuka kwa ngazi. Hii ni tofauti unatembea tu kuingia

 Ice cave in your room.

 Skate park room.



 Backyard office.

 Indoor slide....... mko ndani lakini mnacheza mchezo wa kuslide.

 Kitchen table tennis.


No comments:

Post a Comment