Unaambiwa maisha ni riadha usikubali kushindwa mpaka ufike kwenye finishing line. Tupate maneno ya faraja kutoka kwa watu kadhaa maarufu na waliofanikiwa.
Anaitwa Sandra Day O'connor ana-deal na mambo ya sheria. Anasema Treat people well, dont mislead them. Try to be agreeable as you can be. Try to be helpful rather than harmful.Try to cooperate. Utajenga njia na utafanikiwa. Fanya kitu ambacho kina thamani kukifanya na ndio yalikuwa malengo yake na akafanikiwa.Scott Adam ni Cartoonist yeye anaona kuwa kafanikiwa kwenye vipindi vyake vya katuni kwa kuwa tu anapenda kupendwa so kwa kuwa anapenda kupendwa naye hana budi kupenda wafanyakazi wenzake so always anakuwa a good manager ukijumlisha vyote hivyo maana yake unatengeneza team work nzuri, na always team work means mafanikio!
Huyu jamaa anaitwa Nobu matshuhisa, ni mpishi mahiri wa samaki. Lakini anasema mpaka anatimiza miaka 18 alikuwa hajui chochote kuhusu samaki, lakini akaja mtu akamfundisha vitu baadhi kuhusu samaki. Akaanza kazi kwenye restaurant! Lakini cha ajabu katika miaka mitatu ya kwanza hakujua chochote kuhusu mapishi zaidi ya kujua kuosha vyombo na kusafisha samaki. Lakini kila siku aliendelea kuuliza vitu mbalimbali vinavyohusiana na mapishi ya samaki, na alijibiwa sahihi. Uvumilivu wake na kupenda kwake kujifunza kwa kuuliza kumemfanya leo kuwa mmoja wa wapishi mahiri kabisa duniani wa vyakula vyote hususani samaki!!
Ni mtangazaji mahiri wa Television mwenye kipindi kinaitwa Saturday night live huko nchini marekani, anaitwa Lorne Michaels Hana mengi anasema alipogundua ana kipaji hakuwahi kupumzika, alikifanyia kazi bila kupumzika mpaka alipofanikiwa. Sio eti unajiona una kipaji basi ndio unarelax eti kipaji kitakubeba, utafail.
Nani asiyemjua Russell Simons dunia nzima ya HIP HOP inamtambua na kumuheshimu. Anasema, Every creative idea, every second of happiness, is from stillness. But the way you move around, the world has nothing to do with the stillness in your heart, thats why we have to practice. Kikubwa jamaa hapendi udhulumaji na anahisi ni njia sahihi ya mafanikio yake.
Huyu jamaa anaitwa Arnold palmer ni mchezaji wa Golf. Kuna siku alikuwa kwenye mashindano. Alikuwa akielekea kwenye shimo ili afunge tu na kuchukua ubingwa wa masters, na mpira ulikuwa pembeni kidogo tu ya shimo. Wakati anaenda kupiga kuna jamaa akapayuka kwa kufaraha huku akilitaja jina la Arnold. Aliacha kupiga ule mpira na kwenda kushangilia kidogo na yule jama kisha akarudi ili apige, na alipopiga akakosa na ubingwa ukaota mbawa hapo hapo. Kwa kifupi anatupa funzo usianze kushangilia kabla hujafanikisha hata kama uko karibu kiasi gani kufanikisha. Kwa maneno yake mwenyewe anasema, "I was told all my life not to accept congratulations untill i'ts over!
Mwanamashairi Maya Angelou. Kifupi anazungumzia ni kuacha ubinafsi kama unataka kuwa kiongozi bora. Anasema tusivunjane moyo kwa lolote tunalofanya. Anasema, "No one is not born with courage. Each one develops it by doing small courageous things".
Designer phillipe starck. Kikubwa anatufundisha jinsi ya kujitoa kwa moyo wote kwa kile unachokipenda au unachokifanya. Ndio maana anakuambia amesaini mkataba na shetani hata kama ni kuuza maisha yake ili mradi tu afanye kazi za ubunifu!
Raisi wa zamani wa marekani. Anasema ni bora ufanye kazi yako kuliko kufanya kitu ili ubaki na kazi yako. "I have prepared to criticize even the United states after 9/11 (September eleven bombings). People told me it would not help my career as high commissioner, but it seemed much more important to do the job than to try to keep the job."
Mwanahistoria David McCullough, yeye simple tu anasema usibweteke hakuna kitu rahisi, piga kazi!
No comments:
Post a Comment