LOGO

LOGO

Wednesday 11 November 2015

Hotel ya Kuenjoy!!

Kuenjoy katika hoteli zilizopo visiwani sio tena ufahari ambao matajiri peke yao wanaweza kufaidi, hata watu wa kawaida nao wanaweza cha msingi ni kujipanga tu. Mfano ni hii hoteli ya The Song Saa Private Island Hotel!

Ni kama kitu cha kutengeneza kwenye movie, hoteli hii ya aina yake ipo katikati ya mlima na bahari kwenye ghuba ya Thailand.



The Song Saa Private Island ni moja kati ya visiwa vya Koh Rons, pembeni pembeni ya pwani ya Cambodia na ina View yake itakayokufanya usisimke na mtu yoyote mwenye pesa ya kutumia ni ruksa kwenda.
 


Kila kitu kuhusu eneo hili ni superbly, kuanzia fukwe zake nzuri mpaka maji yake ya bahari yaliyo safi(Blue water), na pia uzuri na usasa wa hoteli yenyewe.


 
Ikiwa na villas 26 zenye muonekano ambao hauwezi kukosa utakapozungumzia muonekano wa kisasa kabisa kwenye magazeti, kila chumba kina pool lake binafsi pamoja na bafu la nje.


 
Michezo ya nje pia ipo, beach ndio usiseme.Kama diving, snorkeling na mingineyo. The Song Saa Private Island Eco Hotel, si mchezo!!!

Mario Balotelli Kwa mabinti!!

Pamoja na utukutu wake uliopitiliza uwanjani na nje ya uwanja, lakini bado hili halimzuii Mario Balloteli mwanasoka mahiri raia wa Italia, kupata warembo bomba kama wapenzi wake. Sasa sijui ni kwa ajili ya pesa au wanamzimikia tu kutokana na Utukutu wake. Na yeye kwa kulijua hilo naona kaamua kuwakomesha, hii ni list ndefu ya mabinti ambao walishawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Mario balloteli.
  Italian Actrees.......Barbara Guerra

 Greek Model...Betty kourakou

Italian model.....Dayane mello
 
 Miss Italy finalist 2010....Melissa castagnoli

English model.....Sophie Reade

 Long distance ranner.......Sara galimberti

 Italian showgirl....Raffaela Fico

 Chloe evans

A hooker.....Jenny Thompson

English model.......Desiree Busetto

 French model.......Vanessa Lawrence

Eliana cartella

Tabby Brown

Model....Fanny Naguesha
 
Veronica Angeloni

 Veronica Graf

Sarra Tommasi 

 Carla howe

Lauren throne

Holly henderson

Ideas za kupiga picha!!

Gobe Mc Clintock ni mpiga picha raia kutoka Canada katika mji wa Calgary ambaye anafanya mfululizo wa picha za kustua za harusi huko Iceland.
 
Akiwa amelipwa na Sarh na Josh, ambao walikuwa wamepanga kufanya sherehe ndogo tu ya harusi pamoja na familia zao na rafiki zao wa karibu huko Ohio, lakini Gabe Mc clintock yeye aliwafanyia kitu tofauti kwa kwenda kuwapiga picha za harusi sehemu tofauti kabisa na zilizozoeleka.
 
Iceland inajulikana kwa landscape yake ya asili iliyo tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani, kwa hiyo haikushangaza hali hiyo kumfanya Gabe Mc clintock kuitumia ipasavyo sehemu hiyo kwa matukio ya picha.
 
Kwa uamuzi huo Sarah na Josh walisema, "ndio, marafiki zetu ni wa kuvutia na wamefanya mambo mengi mazuri kwenye maisha yetu, lakini harusi ilikuwa ni yetu kuifanya na kuitunza mioyoni mwetu. Tukaamua kwamba kama tukitumia pesa nyingi kwa ajili ya harusi yetu, basi hiyo itumike zaidi kwenye kumbukumbu yao." Na ndio maana wakaamua kuteketeza pesa kutoka Ohio kwenda Iceland kwa ajili tu ya kwenda kupiga picha milimani, kwa ajili ya kumbukumbu ya harusi yao!!!!

Friday 23 October 2015

Linaitwa "The heat."

Kwa wale walio na pesa ya kuchezea hususani wapenda kusafiri popote pale duniani, basi nalileta kwenu nyumba ya kifahari itembeayo.(Luxury mobile home).

Ni basi liitwalo 'The heat', ambalo ndani yake lina kila kitu kinachotakiwa kuwepo kwenye nyumba yoyote iliyokamilika na kujitosheleza.

Ni basi la ghorofa mbili ambalo kama utahitaji kwa ajili ya kulikodi kwa ajili ya safari zako mbalimbali aidha za utalii au kula raha tu huku ukizunguka maeneo mbalimbali, basi linapatikana kupitia kampini ya Anderson mobile estates, ni mkwanja wako tu!!

Ni basi lenye masterbedroom, vyumba kadhaa vya wageni, mabafu kadhaa na jiko lililokamilika kwa kila kitu.

Kama mpenzi wa kusafiri kwa nini uhangaike kutafuta vyumba vya hoteli, wakati unaweza tu kuishi kwenye hoteli inayotembea muda wowote utakaotaka wewe?


Inaweza ikawa gharama kubwa, lakini itakufanya ujisikie huru huku ukijua kuwa muda wowote ni just kuweka switch on tu na kwenda mahala pengine!!!

Wednesday 21 October 2015

Flaviana Matata...Matata kama jina lake!

Flaviana matata ni mrembo wa kitanzania, aliyezaliwa tarehe 09 June 1988, mkoani Shinyanga nchini Tanzania. Ni mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu huko Arusha akichukua masomo ya electrical engineering kabla ya kuitupa chini fani hiyo na kujikita kwenye fani ya urembo akijishughulisha zaidi na kazi ya modelling, akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 9, nywele nyeusi na macho ya brown.
Safari yake ya mafanikio katika modelling ilianza pale aliposhiriki shindano la kwanza kabisa la miss universe  Tanzania mwaka 2007 na kuwa mshindi wa kwanza hivyo kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika shindano la dunia la miss universe mwaka huo huo wa 2007. Huko alishiriki na alifanikiwa kuingia katika kundi la mwisho la washiriki 15 (Top 15 semifinalist). Na hapo ndipo milango ilipofunguka kwa kujulikana zaidi Tanzania, afrika na duniani kwa ujumla na ukawa ndio mwanzo wa deals mbalimbali kumuangukia.
Alifanikiwa kufanya tangazo la kuchapisha la modelling kwa ajili sherri hill. Na mwaka 2011 alishinda taji taji la model of the year wa jarida la Arise magazine katika Lagos fashion week. Pia ametokea katika magazine mbalimbali maarufu duniani  kama Dazed&comfused, Glass magazine, L'official na i-Dmagazine.

Amefanya pia catwalk kwa ajili ya brands za wabunifu maarufu kama mustafa hassanali, Vivienne westwood, Tory burch suno na Loiise gray.

Mwenyewe akijielezea alipohojiwa na mtandao mmoja anasema, "mimi ni fundi umeme kama kitu nilichosomea, lakini pia ni Top model nchini mwangu. Naamini kwamba mungu ameniumba kiusahihi na asilia haswa, na ni mwanamke asilia wa kiafrika." Na kweli hakuna wa kupingana na kauli yake, Flaviana matata ni mwafrika haswa kwa mwonekano. Asilia na halisi!!

Mama yake alifariki kwa ajali ya Mv Bukoba katika ziwa Victoria nchini Tanzania, wakati huo Flaviana matata akiwa na umri wa miaka 9  tu.

Kifo hicho ndicho kilichomsukuma mwaka 2011 kuanzisha Flaviana matata Foundation kama kumbukumbu kwa mama yake, mfuko unaojishughulisha na elimu na maendeleo ya mtoto wa kike nchini Tanzania.
Akiizungumzia Tanzania anasema, nafikiri Lushoto, huko kwenye milima ya usambara ni siri iliyojificha ukizungumzia utalii wa Tanzania. Ni sehemu iliyo juu ya milima, ni mji uliotengenezwa na wakoloni wa kijerumani na ni kama Uswisi ukizungumzia muonekane wake. Hali ya hewa imepoa."


Flaviana matata ameolewa na kijana mmoja mtanashati anayeitwa Deo Massawe!