LOGO

LOGO

Tuesday, 10 February 2015

Mambo ya msingi wapenzi wanayotakiwa kuyajua kwenye mahusiano!

Ili kuwa na mahusiano bora na ya furaha muda wote wa uhusiano wenu wewe na mpenzi wako, iwe mume/mke, au boyfriend/girlfriend, basi bila couple lazima ijue vitu vingi vya muhimu kuhusu mahusiano, vitu ambavyo kama vitafuatwa na kutiliwa mkazo basi ni kujiweka kati nafasi nzuri ya kufurahia mahusiano yenu. Kwa kawaida tunapata ujuzi na uelewa wa mambo haya kutokana na uzoefu wa kote tulipowahi kupita huko siku za nyuma, lakini inafika hatua inabidi kukubali ukweli kuwa sisi wenyewe tunaweza kuweka mambo sawa sasa bila kuangalia nyuma ingawa experience ya nyuma inaweza pia kusaidia ya sasa.

1.Ukarimu.
Siku hizi ukarimu unaonekana kuwa kwa watu wachache sana. Yote inasababishwa na ubize katika maisha au ugumu wa maisha, kiasi kwamba tunasahau kuwa wakarimu kwa baadhi ya mambo. Haihitaji nguvu nyingi kuwa mkarimu, ni kiasi cha kujizoesha tu tu kuwa na tabia hiyo.

Kama utachagua kuwa mkarimu, utagundua na kukubali ni nini nguvu ya ukarimu katika mahusiano. Una faida kubwa kwenye mahusiano, na unaweza kuufanya uhusiano wako kuwa thabiti, madhubuti,imara na wenye afya ambavyo ukivijumlisha vyote hivyo jibu lake litakuwa ni uhusiano wenye furaha. Ukiwa makarimu itasababisha uwe akilini na moyoni mwa mwenza wako muda wote. Muda wote atakaa akikumbuka ukarimu wako, na kitendo cha kukumbuka ukarimu wako, maana yake atakukumbuka wewe,na akikumbuka wewe, ndio mwanzo wa kuwa mawazoni mwake muda wote.

2.Kila mtu huwa na siku mbaya.
Usipende kuchukulia siku mbaya(Bad mood) ya mwenza wako katika baadhi ya siku kuwa ni kwa ajili yako(Don't take it personal). Lazima utambue kila mtu huko anapopita iwe kazini au njiani, lazima atakutana na maudhi yanayoweza kumuharibia siku yake. Huwezi kujiingiza t kwenye masuala yote ya mwenza wako na ni ngumu kujua yaliyomsibu huko alokotoka, cha msingi mliwaze na mpe moyo na mruhusu apambane na yanayomsibu. Narudia don't take it personal.

3.Msigombane/kubishana hadharani.
Ni ukweli ulio wazi kwamba uhusiano thabiti, madhubuti na wa kudumu lazima kuwepo kwa kutokukubaliana kwa baadhi ya mambo muda Fulani, au kwa lugha nyingine lazima kuwepo kwa kupishana aidha kwa maneno au kwa vitendo. Hapa sasa ndipo hutokea mabishano ya kila mtu kutaka kuuonyesha mwenzake kwamba yeye ndio yupo sahihi. Ni sawa, lakini msifanye hivyo hadharani. Kama imetokea mmepishana kitu fulani, msigombane au kubishana hadharani, nendeni nyumbani, tulieni, ongeeni na muwekane sawa..(Don't wash your dirty linen in public!).

4.Kucheka/kufurahi pamoja ni muhimu.
Furaha, haswa haswa kucheka hutibu mioyo na kuunganisha watu. Kucheka kuna uwezo mkubwa wa kuvunja vikwazo vya ndani, mawazo, uoga na kukufanya uwe huru na mwenye furaha. Utani mzuri wa mara kwa mara unarahisisha wenza kuwa pamoja na kuweka mambo yao pamoja kirahisi.

5.Kusameheana.
Mkiwa kwenye uhusiano na mwenzako na mkajenga tabia ya kusameheana, basi mnajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa katika uhusiano wa muda mrefu, thabiti na wenye afya.
Wote mnaweza kufanya kufanya makosa na njia rahisi ya kuwekana sawa ni kwanza kukubali kuwa kweli nimekosea. Cha pili ni kilichopita, kiachwe kipite. ukikumbuka makosa yaliyopita, utazima msisimko wote wa mapenzi ya sasa hivi. Furahia mahusiano yako na maisha yako kadri uwezavyo na samehe makosa, utafurahia mapenzi maisha yako yote.

6.Wasilianeni vizuri na kwa uwazi.
Utagundua kwamba watu wengi huwa hawawezi kusoma mawazo ya mwenzake. Watu walio kwenye uhusiano mara nyingine wanashindwa kuwa katika uhusiano mzuri kwa kuwa tu wanashindwa kusoma mawazo mwenzake.

Kwa nini tunahitaji kusoma mawazo ya wenzetu? Jibu ni rahisi. Itarahisisha kuwasiliana vizuri na kwa uwazi. Itaokoa muda na nguvu ya kumjua mwenzako. Hakuna haja ya kuwasiliana kwa mafumbo na mwenzako, ongea kitu unachodhamiria kusema. Mawasiliano mazuri hustawisha uhusiano.

7.Jifunge/Jitoe.
Kujitoa kwa mwenza wako kunadhihirisha upendo wako wa dhati kwake na kunaonyesha umuhimu wako kwake. Wakati thamani ya kujitoa kwako ikionekana, ni wazi unatengeneza nafasi moyoni kwa mpenzi wako. Kujitoa na kujifunga kwa mwenzako ni sehemu muhimu sana kwenye uhusiano. Ingawa sio kwa maneno bali kwa vitendo.

Mapenzi au mahusiano, ni suala pana sana linalohitaji umakini mkubwa kuweza kutengeneza penzi lenye furaha, amani na upendo. Unaweza ukawa na njia nyingine nyingi za ziada lakini kupitia hizi chache zilizoorodheshwa hapo juu, hakika utaenjoy your love, utam-enjoy partner wako na utakuwa na uhakika wa a lasting relationship!

The King Mayweather!!

Kama eti unajiita mpenzi wa mchezo wa ngumi(Boxing), au mfuatiliaji wa mchezo wa ngumi, halafu eti ukasema hujawahi kumsikia bondia anayeitwa Mayweather,Jr, basi wewe utakuwa una mapepo na unahitaji kupepewa.

Jina lake kamili anaitwa Floyd Mayweather,Jr, kipande cha baba kilichozaliwa tarehe 24 February 1977 huko Grand Rapids,Michigan, nchini Marekani, huku akijulikana kwa jina la utani la Pretty boy money. Ana urefu wa futi 5 na inchi 8 ambao ni sawa na mita 1.73.


Amekuwa ni bondio asiyepigika kwa miaka mingi tokea aanze mchezo wa ngumi huku akiwa amewahi kutwaa mikanda ya dunia zaidi ya nane katika uzito tofauti tofauti. Ameshakuwa bondia bora wa mwaka mara mbili wa jarida la Ring(Mwaka 1998 na 2007), ameshachaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka(2007) na waandishi wa habari za boxing nchini marekani na pia mpiganaji bora wa tuzo za ESPY katika miaka ya 2007,2008,2010,2012 na 2013.
 

Ameshakuwa bingwa wa dunia wa WBC welterweight, WBA super welterweight, WBC superelterweight naWBC diamond super welterweight. Na pia anatajwa kuwa ndiyo mfalme wa "pound for pound" duniani, aina ya kupigana ambayo bondio muda wote anakuja tu na kurusha ngumi bila kurudi nyuma na hiyo ni kwa mujibu wa vyombo karibu vyote vikubwa vya michezo duniani kama Ring,Sports illustrated, ESPN,Box rec,Fox sports na Yahoo sports, na kwa miaka mingi amekuwa akitawala kama mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kuliko mwanamichezo yoyote duniani.
 

Kama ilivyoandikwa awali,alizaliwa Grand rapids,Michigan, katika familia ya wanamasumbwi kwani baba yake mzazi Floyd mayweater Sr, alikuwa ni bondia na aliwahi kupigana hata na bondia Sugar Ray Leonard. Wajomba zake wawili Jeff Mayweather na Roger mayweather wote walikuwa ni mabondia wa kulipwa kabla ya Roger ambaye aliwahi kutwaa mataji mawili ya dunia, kuwa mwalimu wa Floyd hapo baadaye.

 
Mchezo wa ngumi umekuwa ni sehemu ya maisha ya Mayweather tangu akiwa mtoto na hajawahi kujaribu shughuli au kazi nyingine yeyote.

Aliwahi kusema,"nafikiri bibi yangu alikuwa wa kwanza kugundua kipaji change. Kwani kuna siku nilipokuwa mdogo, nilimwambia kuwa inabidi nitafute kazi na alinijibu, hapana endelea kucheza Boxing. Nilipokuwa ni miaka tisa, niliishi New jersey pamoja na mama yangu na watu wengine saba katika chumba kimoja na muda mwingine kikiwa hakina umeme." Aliendelea kuhadithia mayweather,"watu wakiona nilicho nacho sasa, huwa hawana picha ya wapi nilipotokea nikiwa sina chochote cha kunisaidia kukua."

Ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mayweather kurudi nyumbani kutoka shuleni na kukuta sindano zilizotumika kujidungia dawa za kulevya zikiwa zikiwa zimetapakaa kibarazani kwao. Hiyo ni kwa sababu hata mama yake mzazi alikuwa ni mwathirika wa dawa za kulevya, na pia alikuwa na shangazi yake ambaye alifariki kutokana na ukimwi uliosababishwa na kushare sindano wakati wa kutumia madawa ya kulevya. "Watu hawaelewi nimepitia maisha ya ajabu kiasi gani." Alizidi kufafanua Mayweather.


Katika makuzi yake, muda ambao baba yake alitumia kuwa naye ilikuwa ni wakati wa kumpeleka Gym kufanya mazoezi na kujishughulisha na mchezo wake wa ngumi tu basi. Anasema,"Sikumbuki kama baba aliwahi kunipeleka au kunifanyia kitu ambacho kama mzazi alitakiwa amfanyie mwanaye. Kwa mfano kuangalia wanyama, au kwenda kuangalia sinema au kwenda kula Ice Cream." Anaendelea,"siku zote niliamni alimpenda zaidi mtoto wake wa kike(Dada yake wa kambo Mayweather), zaidi ya alivyonipenda mimi".


Lakini baba yake Mayweather anajitetea kwa kusema mwanaye hasemi ukweli na kusema kuwa alikuwa baba bora ambaye hakupenda mwanaye apotee."Pamoja nilikuwa nauza madawa ya kulevya, sikuwahi kumshawishi, ingawa alikuwa sehemu ya maisha hayo. Siku zote alikuwa akipata chakula cha kutosha, siku zote nilimnu nilimnunulia nguo nzuri na nilikuwa nikimpatia nikimpatia pesa ambazo alikuwa hata hana mahitaji nazo. Mtu yoyote pale Grand Rapid(Eneo walilokuwa wanaishi), ukimuuliza atakuambia kwamba nilikuwa naijali familia yangu.Siku zote nilijitahidi kuhangaikia maisha muda wa usiku na kuhakikisha muda wa mchana nakuwa naye, kumpeleka Gym na kumfundisha kuwa boxer. Kama nisingekuwa mimi, asingekuwa hapo alipo leo". Alimaliza baba yake Mayweather.


Lakini mayweather bado aliweka msimamo, "Kimsingi nilijikuza mwenyewe. Bibi yangu alijitahidi kufanya yote aliyoweza kufanya kunikuza. Na muda mwingine aliponigombeza nilikwenda kwa mama yangu. Maisha yalikuwa ni ya milima na mabonde".

Boxing ndio njia iliyomtoa Mayweather. Ni njia pekee aliyoona sahihi kujishughulisha nayo ili kuondoa mawazo ya kuwa mbali na baba yake. Aliweka nguvu zake zote kwenye boxing, ikiwa pamoja na kuacha shule. Anasema,"Nilijua kuwa nilitakiwa kujaribu kwa namna yoyote kumhudumia mama yangu na nilijiwekea msimamo mwenyewe kwamba shule haikuwa na umuhimu kwa muda ule, ilikuwa nilazima nifanye boxing ili tupate chochote cha kutufanya tuishi."

Na kweli sasa anaishi, tena ni zaidi ya kuishi. Mmiliki huyu wa The money team, huku kauli mbiu yake ikiwa Tough life don't last, tough people do!!!!!

Kama mkwanja upo wa kutosha, hii ndio miji ya kutembelea duniani!!

Mara nyingi watu wanapoenda mapumziko baada ya mihangaiko ya mwaka mzima, aidha kwa kwenda kutalii au kupumzika tu, basi kati ya vitu ambavyo huwa wanaviangalia sana ni baljeti ya safari nzima. Si uongo wala kificho kuwa wengi huangalia na kupanga kwenda sehemu yenye unafuu wa gharama. (Low budget destinations.)

Lakini kuna suala moja, kuna tatizo gani angalau mara moja kati ya miaka kadhaa hivi ukaamua kuchana mfuko na kuamua kula bata haswa(Pamper yourself) katika maeneo luxuries zaidi? Maana ukweli uko wazi, maeneo luxuries huwa ndio salama na mvuto wa pikee. Hebu take time one day vunja akaunti yako na ukajiachie katika miji na maeneo yafuatayo, hutojuta!

1.Monaco.
Ni mji mdogo unaopatikana kwenye pwani ya ufaransa. Monaco ni maarufu kwa film festival na vitu vitu vya gharama na anasa. Wanasema kila mtu anayeishi Monaco anataka kuishi kifalme, na wanafanya hivyo haswa bila kujinyima. Kuna majumba na magari ya kifahari, maduka ya kushangaza na migahawa ya hali ya juu inayofanya mji wa Monaco kuwa mji wa kifahari ambao kama hali yako ya kifedha inakuruhusu basi usisite kuutembelea.

Hoteli nyingi mjini Monaco ni ghali sana ingawa utapata huduma ya hali juu na utakuwa confortable kiasi kwamba hutokumbuka wala kujutia kiasi ulichotumia.

2.French Polynesia.
Ni mji unaojulikana kama Tahiti. French Polynesia ni paradise ya ukweli, iliyoko kusini mwa bahari ya pacific. Kuna bungallows ambazo ziko kwa juu milimani kuzunguka bahari na ndipo accomodations nyingi zinapopatikana kama ukitembelea sehemu hii, ambapo utapata private villas zenye mandhari nadhifu, huku ukiletewa breakfast kwenye kibaraza chako ili upate kifungua kinywa huku ukitazama mandhari ya bahari kwa chini.

Pamoja kuwa French Polynesia ni sehemu ya kufikia kwa ajili ya kurelax, lakini pia kuna vitu vingine vingi vya kuvutia vya kufanya pale, hususani kwa wapenzi wa michezo ya kwenye maji.(Water sports).

3.Dubai.
Dubai ni kati ya sehemu ambazo kila mtu anaota kupatembelea angalau maramoja katika uhai wake. Ni moja kati mji wa kuvutia duniani uliofurika majengo marefu(Sky scrapers), Hotels za hali ya juu. Na usishangae, ndio mji wenye maduka makubwa ba ghali zaidi duniani kwa ajili ya shopping. (The world's most expensive and biggest shopping malls).

Wakati nchi nyingi umezoea kusikia wana 5 star hotels, lakini Dubai inajulikana kwa kuwa na Hoteli ya nyota 7 (7 star hotel), yenye vyumba vya mpaka kifalme sio presidential suits tu, vyumba ambavyo vinafikia mpaka dola 10,000 kwa usiku mmoja.

Ni mji maarufu wa wasafiri wa kibiashara na watalii amabo wanamudu gharama za mji huu.

4.Maldives.
Ni moja ya miji mizuri sana kama unataka kwenda for honeymoon. Maldives inakumuisha visiwa mbalimbali ambavyo vyote vina mvuto wa kipekee.

Waansema watu wanaoishi hapa wanatengeneza fedha nyingi sana, na nyingi kati ya hizo zinatokana na utalii na shughuli za uvuvi. Kutokana na kipato kuwa kikubwa, ndicho kinachofanya bei za migahawa na hotels nazo ziwe juu sana pia.

5.Singapore.
Miaka michache nyuma Singapore ilikuwa ni sehemu amabayo unaweza kufikia kwa gharama za kawaida kabisa, lakini kwa kasi ya hali ya juu pamegeuka kuwa a true luxury destination. Imejenga estates, hotels za luxury, shopping malls na migahawa mingi yenye hadhi ya dunia.(World class restaurants). Inakadiriwa vyumba vya hotel za wastani ni dola 200 kwa siku. Ni sehemu nzuri kutembelea kama umejipanga kutuonea huruma mfuko wako wa fedha.

6.Japan.
Unaweza ukajiuliza na kushangaa kuona Japan imeingiaje kwenye List hii ya luxury destinations, lakini ukweli unabaki kuwa ndio huo kuwa ni mahali pa gharama kubwa kupatembelea. Ni mahali sahihi kama unataka kufanya vacation ya gharama. Hata kama utataka kufikia katika hotels za gharama ya wastani, bado itabidi uwe na si chini ya dola 250 kwa usiku mmoja.

Kuna vitu vingi vya kufanya ukiwa Japan, so sio sehemu ambayo utakuwa boered. Kuna miji mingi yenye uzuri wa kushangaza, mambo mengi matamu ya utamaduni, fukwe za kuvuti na mandhari adimu za milima.

Usihofu kama hujui kuzungumza Kijapani, utatumia ishara za mikono tu kuwasiliana na wenyeji, maana hawa jamaa wengi wao hawajui kiingereza!!!

7.Fiji.
Fiji ni maarufu kwa kutembelewa na wageni kutoka Australia, New Zealand na marekani. Pamoja na Fiji kuwa mara zote imejaza watalii, lakini siku zote imekuwa ni sehemu ya amani, huku shughuli za honeymoon zikiwa ndio mahala pake haswaa.

Ina milima miangavu ya kijani, fukwe za michanga myeupe(White sandy beaches). Hoteli zake ni za kisasa na luxury haswa, pia ziko romantic na kuna mengi ya kufanya hususani ukiwa mpenzi wa michezo ya kwenye maji.

Na kama unataka kujifunza mambo ya utamaduni, basi usiache kutembelea baadhi ya vijiji hapo Fiji, utafurahi.

Fiji ina shughuli nyingi za kustaajabisha(Adventure activities), zitkazokustua na kumvutia kila mtu atakayebahatika kufika pale!!

Monday, 9 February 2015

Unajua kwa nini Jokate anapapatikiwa na wanaume? Mwenyewe aelezea....

Ni mshindi wa miss Temeke mwaka 2006, ushindi uliompa Ticket ya kushiriki Miss Tanzania ingawa hakubahatika kuwa mshindi, alishika nafasi ya pili, ila alifanikiwa kuutwaa ubalozi wa bia ya Redds. Hapa namzungumzia Jokate Mwegelo....

Pamoja na kutoshinda taji la Miss Tanzania mwaka huo lakini kushiriki kwake tu ilikuwa kama ndio mlango umefunguliwa wa mafanikio katika Nyanja nyingine. Kwani baada ya hapo aligeukia filamu akiigiza movie kama fake pastors na chumo, akaingia kwenye music na kufanya vizuri ingawa sio sana.


Akaingia pia kwenye suala la endeshaji shughuli, "msema chochote", shughuli za U-Mc. Hapa amefanikiwa sana kwani amefanikiwa kuongoza shughuli nyingi kubwa za tuzo au sherehe mbalimbali na hivyo kujiingizia mkwanja wa kutosha.


Kubwa jingine lenye mafanikio ni suala la mitindo, ameshika sana eneo hili. Unapomzungumzia Jokate na mitindo basi lazima uzungumzie Kidoti. Kidoti ni brand ya mitindo inayomilikiwa na Jokate mwenyewe. Humo utakutana na nywele, mavazi na sandals. Kidoti ni brand inayozidi kumfungulia njia ya mafanikio kimataifa, kiasi cha kupata deal na wachina, deal lililomuingizia billions of money, sizungumzii milioni hapa, ni billions.


Upande wa modeling naye yumo, mara kwa mara amekuwa akionekana kwenye matukio mbalimbali akifanya catwalks na vitu kama hivyo. Mfano alishawahi kushiriki onesho la mitindo la Red Ribbon lililokuwa maalumu kwa kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto walioathirika na ugonjwa wa ukimwi chini ya taasisi T anzania mitindo house iliyo chini ya mwenyekiti, Khadija mwanamboka.

Lakini pia ni mtangazaji wa TV kitaifa na kimataifa. Kitaifa amefanya kazi na TV1 wakati kimataifa ametusua mpaka pande za kwa mzee madiba na kufanya kazi na kituo bora kabisa cha televisheni duniani, channel O.


Anyway yote kwa yote amewahi kuzungumzia kidogo kuhusu suala la mapenzi. Aliongelea tu kwa nini wanaume wengi humpapatikia yeye?

1.Kujiamini.
Anasema hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Na yeye anasema kuwa  ni wanamke anayejiamini sana that why midume inawatoka midenda!


2.Kujitegemea.
Anasema hii nayo inafanana na suala la kujiamini. Anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama kuwa na mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume kuwa wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana.


3.Kupendeza.
Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa nguo zenye rangi ya kuonekana. Hapa akitaja sila yake mojawapo ya kupendwa kuwa ni kupendeza kwake.


4.Tabasamu.
Sio kila saa unanuna tu, Tabasamu. Jokate anasema ukitabasamu kila saa, tabasamu hilo linakufanya unaonekana ni mzuri zaidi.


Kazi kwenu wadada, mwenzenu anaamini katika mambo hayo manne yanayosababisha wanaume wapigane vikumbo kwake!!