LOGO

LOGO

Tuesday 10 February 2015

The King Mayweather!!

Kama eti unajiita mpenzi wa mchezo wa ngumi(Boxing), au mfuatiliaji wa mchezo wa ngumi, halafu eti ukasema hujawahi kumsikia bondia anayeitwa Mayweather,Jr, basi wewe utakuwa una mapepo na unahitaji kupepewa.

Jina lake kamili anaitwa Floyd Mayweather,Jr, kipande cha baba kilichozaliwa tarehe 24 February 1977 huko Grand Rapids,Michigan, nchini Marekani, huku akijulikana kwa jina la utani la Pretty boy money. Ana urefu wa futi 5 na inchi 8 ambao ni sawa na mita 1.73.


Amekuwa ni bondio asiyepigika kwa miaka mingi tokea aanze mchezo wa ngumi huku akiwa amewahi kutwaa mikanda ya dunia zaidi ya nane katika uzito tofauti tofauti. Ameshakuwa bondia bora wa mwaka mara mbili wa jarida la Ring(Mwaka 1998 na 2007), ameshachaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka(2007) na waandishi wa habari za boxing nchini marekani na pia mpiganaji bora wa tuzo za ESPY katika miaka ya 2007,2008,2010,2012 na 2013.
 

Ameshakuwa bingwa wa dunia wa WBC welterweight, WBA super welterweight, WBC superelterweight naWBC diamond super welterweight. Na pia anatajwa kuwa ndiyo mfalme wa "pound for pound" duniani, aina ya kupigana ambayo bondio muda wote anakuja tu na kurusha ngumi bila kurudi nyuma na hiyo ni kwa mujibu wa vyombo karibu vyote vikubwa vya michezo duniani kama Ring,Sports illustrated, ESPN,Box rec,Fox sports na Yahoo sports, na kwa miaka mingi amekuwa akitawala kama mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kuliko mwanamichezo yoyote duniani.
 

Kama ilivyoandikwa awali,alizaliwa Grand rapids,Michigan, katika familia ya wanamasumbwi kwani baba yake mzazi Floyd mayweater Sr, alikuwa ni bondia na aliwahi kupigana hata na bondia Sugar Ray Leonard. Wajomba zake wawili Jeff Mayweather na Roger mayweather wote walikuwa ni mabondia wa kulipwa kabla ya Roger ambaye aliwahi kutwaa mataji mawili ya dunia, kuwa mwalimu wa Floyd hapo baadaye.

 
Mchezo wa ngumi umekuwa ni sehemu ya maisha ya Mayweather tangu akiwa mtoto na hajawahi kujaribu shughuli au kazi nyingine yeyote.

Aliwahi kusema,"nafikiri bibi yangu alikuwa wa kwanza kugundua kipaji change. Kwani kuna siku nilipokuwa mdogo, nilimwambia kuwa inabidi nitafute kazi na alinijibu, hapana endelea kucheza Boxing. Nilipokuwa ni miaka tisa, niliishi New jersey pamoja na mama yangu na watu wengine saba katika chumba kimoja na muda mwingine kikiwa hakina umeme." Aliendelea kuhadithia mayweather,"watu wakiona nilicho nacho sasa, huwa hawana picha ya wapi nilipotokea nikiwa sina chochote cha kunisaidia kukua."

Ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mayweather kurudi nyumbani kutoka shuleni na kukuta sindano zilizotumika kujidungia dawa za kulevya zikiwa zikiwa zimetapakaa kibarazani kwao. Hiyo ni kwa sababu hata mama yake mzazi alikuwa ni mwathirika wa dawa za kulevya, na pia alikuwa na shangazi yake ambaye alifariki kutokana na ukimwi uliosababishwa na kushare sindano wakati wa kutumia madawa ya kulevya. "Watu hawaelewi nimepitia maisha ya ajabu kiasi gani." Alizidi kufafanua Mayweather.


Katika makuzi yake, muda ambao baba yake alitumia kuwa naye ilikuwa ni wakati wa kumpeleka Gym kufanya mazoezi na kujishughulisha na mchezo wake wa ngumi tu basi. Anasema,"Sikumbuki kama baba aliwahi kunipeleka au kunifanyia kitu ambacho kama mzazi alitakiwa amfanyie mwanaye. Kwa mfano kuangalia wanyama, au kwenda kuangalia sinema au kwenda kula Ice Cream." Anaendelea,"siku zote niliamni alimpenda zaidi mtoto wake wa kike(Dada yake wa kambo Mayweather), zaidi ya alivyonipenda mimi".


Lakini baba yake Mayweather anajitetea kwa kusema mwanaye hasemi ukweli na kusema kuwa alikuwa baba bora ambaye hakupenda mwanaye apotee."Pamoja nilikuwa nauza madawa ya kulevya, sikuwahi kumshawishi, ingawa alikuwa sehemu ya maisha hayo. Siku zote alikuwa akipata chakula cha kutosha, siku zote nilimnu nilimnunulia nguo nzuri na nilikuwa nikimpatia nikimpatia pesa ambazo alikuwa hata hana mahitaji nazo. Mtu yoyote pale Grand Rapid(Eneo walilokuwa wanaishi), ukimuuliza atakuambia kwamba nilikuwa naijali familia yangu.Siku zote nilijitahidi kuhangaikia maisha muda wa usiku na kuhakikisha muda wa mchana nakuwa naye, kumpeleka Gym na kumfundisha kuwa boxer. Kama nisingekuwa mimi, asingekuwa hapo alipo leo". Alimaliza baba yake Mayweather.


Lakini mayweather bado aliweka msimamo, "Kimsingi nilijikuza mwenyewe. Bibi yangu alijitahidi kufanya yote aliyoweza kufanya kunikuza. Na muda mwingine aliponigombeza nilikwenda kwa mama yangu. Maisha yalikuwa ni ya milima na mabonde".

Boxing ndio njia iliyomtoa Mayweather. Ni njia pekee aliyoona sahihi kujishughulisha nayo ili kuondoa mawazo ya kuwa mbali na baba yake. Aliweka nguvu zake zote kwenye boxing, ikiwa pamoja na kuacha shule. Anasema,"Nilijua kuwa nilitakiwa kujaribu kwa namna yoyote kumhudumia mama yangu na nilijiwekea msimamo mwenyewe kwamba shule haikuwa na umuhimu kwa muda ule, ilikuwa nilazima nifanye boxing ili tupate chochote cha kutufanya tuishi."

Na kweli sasa anaishi, tena ni zaidi ya kuishi. Mmiliki huyu wa The money team, huku kauli mbiu yake ikiwa Tough life don't last, tough people do!!!!!

No comments:

Post a Comment