LOGO

LOGO

Tuesday 10 February 2015

Mambo ya msingi wapenzi wanayotakiwa kuyajua kwenye mahusiano!

Ili kuwa na mahusiano bora na ya furaha muda wote wa uhusiano wenu wewe na mpenzi wako, iwe mume/mke, au boyfriend/girlfriend, basi bila couple lazima ijue vitu vingi vya muhimu kuhusu mahusiano, vitu ambavyo kama vitafuatwa na kutiliwa mkazo basi ni kujiweka kati nafasi nzuri ya kufurahia mahusiano yenu. Kwa kawaida tunapata ujuzi na uelewa wa mambo haya kutokana na uzoefu wa kote tulipowahi kupita huko siku za nyuma, lakini inafika hatua inabidi kukubali ukweli kuwa sisi wenyewe tunaweza kuweka mambo sawa sasa bila kuangalia nyuma ingawa experience ya nyuma inaweza pia kusaidia ya sasa.

1.Ukarimu.
Siku hizi ukarimu unaonekana kuwa kwa watu wachache sana. Yote inasababishwa na ubize katika maisha au ugumu wa maisha, kiasi kwamba tunasahau kuwa wakarimu kwa baadhi ya mambo. Haihitaji nguvu nyingi kuwa mkarimu, ni kiasi cha kujizoesha tu tu kuwa na tabia hiyo.

Kama utachagua kuwa mkarimu, utagundua na kukubali ni nini nguvu ya ukarimu katika mahusiano. Una faida kubwa kwenye mahusiano, na unaweza kuufanya uhusiano wako kuwa thabiti, madhubuti,imara na wenye afya ambavyo ukivijumlisha vyote hivyo jibu lake litakuwa ni uhusiano wenye furaha. Ukiwa makarimu itasababisha uwe akilini na moyoni mwa mwenza wako muda wote. Muda wote atakaa akikumbuka ukarimu wako, na kitendo cha kukumbuka ukarimu wako, maana yake atakukumbuka wewe,na akikumbuka wewe, ndio mwanzo wa kuwa mawazoni mwake muda wote.

2.Kila mtu huwa na siku mbaya.
Usipende kuchukulia siku mbaya(Bad mood) ya mwenza wako katika baadhi ya siku kuwa ni kwa ajili yako(Don't take it personal). Lazima utambue kila mtu huko anapopita iwe kazini au njiani, lazima atakutana na maudhi yanayoweza kumuharibia siku yake. Huwezi kujiingiza t kwenye masuala yote ya mwenza wako na ni ngumu kujua yaliyomsibu huko alokotoka, cha msingi mliwaze na mpe moyo na mruhusu apambane na yanayomsibu. Narudia don't take it personal.

3.Msigombane/kubishana hadharani.
Ni ukweli ulio wazi kwamba uhusiano thabiti, madhubuti na wa kudumu lazima kuwepo kwa kutokukubaliana kwa baadhi ya mambo muda Fulani, au kwa lugha nyingine lazima kuwepo kwa kupishana aidha kwa maneno au kwa vitendo. Hapa sasa ndipo hutokea mabishano ya kila mtu kutaka kuuonyesha mwenzake kwamba yeye ndio yupo sahihi. Ni sawa, lakini msifanye hivyo hadharani. Kama imetokea mmepishana kitu fulani, msigombane au kubishana hadharani, nendeni nyumbani, tulieni, ongeeni na muwekane sawa..(Don't wash your dirty linen in public!).

4.Kucheka/kufurahi pamoja ni muhimu.
Furaha, haswa haswa kucheka hutibu mioyo na kuunganisha watu. Kucheka kuna uwezo mkubwa wa kuvunja vikwazo vya ndani, mawazo, uoga na kukufanya uwe huru na mwenye furaha. Utani mzuri wa mara kwa mara unarahisisha wenza kuwa pamoja na kuweka mambo yao pamoja kirahisi.

5.Kusameheana.
Mkiwa kwenye uhusiano na mwenzako na mkajenga tabia ya kusameheana, basi mnajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa katika uhusiano wa muda mrefu, thabiti na wenye afya.
Wote mnaweza kufanya kufanya makosa na njia rahisi ya kuwekana sawa ni kwanza kukubali kuwa kweli nimekosea. Cha pili ni kilichopita, kiachwe kipite. ukikumbuka makosa yaliyopita, utazima msisimko wote wa mapenzi ya sasa hivi. Furahia mahusiano yako na maisha yako kadri uwezavyo na samehe makosa, utafurahia mapenzi maisha yako yote.

6.Wasilianeni vizuri na kwa uwazi.
Utagundua kwamba watu wengi huwa hawawezi kusoma mawazo ya mwenzake. Watu walio kwenye uhusiano mara nyingine wanashindwa kuwa katika uhusiano mzuri kwa kuwa tu wanashindwa kusoma mawazo mwenzake.

Kwa nini tunahitaji kusoma mawazo ya wenzetu? Jibu ni rahisi. Itarahisisha kuwasiliana vizuri na kwa uwazi. Itaokoa muda na nguvu ya kumjua mwenzako. Hakuna haja ya kuwasiliana kwa mafumbo na mwenzako, ongea kitu unachodhamiria kusema. Mawasiliano mazuri hustawisha uhusiano.

7.Jifunge/Jitoe.
Kujitoa kwa mwenza wako kunadhihirisha upendo wako wa dhati kwake na kunaonyesha umuhimu wako kwake. Wakati thamani ya kujitoa kwako ikionekana, ni wazi unatengeneza nafasi moyoni kwa mpenzi wako. Kujitoa na kujifunga kwa mwenzako ni sehemu muhimu sana kwenye uhusiano. Ingawa sio kwa maneno bali kwa vitendo.

Mapenzi au mahusiano, ni suala pana sana linalohitaji umakini mkubwa kuweza kutengeneza penzi lenye furaha, amani na upendo. Unaweza ukawa na njia nyingine nyingi za ziada lakini kupitia hizi chache zilizoorodheshwa hapo juu, hakika utaenjoy your love, utam-enjoy partner wako na utakuwa na uhakika wa a lasting relationship!

No comments:

Post a Comment