LOGO

LOGO

Saturday 7 February 2015

Kama umeajiriwa, epuka kufanya yafuatayo sehemu yako ya kazi!

Kama unataka kuwa mfanyakazi mwenye mafanikio, amani na furaha sehemu ya kazi basi ni budi kuepuka kufanya mambo Fulani Fulani, labda kama hujali chochote hata kama ukipoteza kazi yako. Siku zote kama unataka kuonekana kuwa uko serious na ajira yako, basi ni lazima ushike sharia za kazi na kuepuka tabia ambazo zinaweza kukwaza wafanyakazi wenzako.

1.Kusengenya/Umbea.
Iliwahi kutamkwa kuwa, "Strong minds discuss ideas,average minds discuss events, weak minds discuss people." Kusengenya mfanyakazi mwenzako au kuendekeza umbea sehemu ya kazi ni tabia ya watu wenye weak minds. Ni sumu mbaya sana kwa ubora na muonekano wako kazini.

Ni vyema ukakwepa kabisa tabia ya kuongelea wafanyakazi wenzako, kwani utajiweka kwenye nafasi ya kutopewa mamlaka au majukumu muhimu na hata kupoteza imani kwa wakubwa zako wa kazi.

Siku zote kumbuka umekwenda kazini kufanya kazi na sio kuzungumzia watu. Unaweza ukawazungumzia watu maisha yao binafsi, kama kuna umuhimu, lakini sio kazini! Kazini ni sehemu ya kuonyesha uhodari wako wa kazi tu.

2.Kutokuwa na morali ya kazi.
Kwa lugha nyingine utasikia mtu anasema,"Leo sina mood ya kazi kweli.". Kutokuwa na morali ya kufanya kazi, limekuwa ni suala lililowazi sehemu nyingi za kazi. Ni mbaya sana kwani husababisha kushusha uzalishaji sehemu ya kazi, hupunguza ushirikiano aidha baina ya mfanyakazi kwa mfanyakazi au idara kwa idara na pia husababisha kuwa na makosa mengi kwenye kazi iliyofanywa na muhusika.

Na kumbukuka ukiendekeza tabia hiyo hutopata heshima stahili toka kwa wafanyakazi wenzako, kila mtu atakutafsiri kama ni mzembe na usiyejituma ni hivyo kupoteza hamu ya kushirikiana na wewe.

Siku zote unapotoka nyumbani kwenda kazini hakikisha mambo ya pembeni au nyumbani unayaweka pembeni na akili yako unaielekeza kwenye majukumu yako ya kazini hiyo itakusaidia kuwa na morali ya juu ya kazi muda wote.

3.Mikwaruzano.
Watu wanaofanya kazi pamoja ni binadamu. Kila binadamu ana hisia tofauti na binadamu mwingine, ana mawazo tofauti na mwingine, ana maono tofauti, ana fikra tofauti na hata maamuzi tofauti, hivyo ni rahisi sana kutokea mikwaruzano sehemu ya kazi kutokana na tofauti hizo.

Inapotokea mikwaruzano, jaribu kwa nguvu na namna yoyote ile kupunguza ukubwa wa mkwaruzano huo pamoja na athari zinazoweza kujitokeza sehemu ya kazi kutokana na kupishana huko. Ukitoa nafasi kwa mikwaruzano sehemu ya kazi, ni dhahiri unapunguza tija kazini.

Moja ya njia sahihi ya kukwepa mikwaruzano ni kupuuza chanzo kukwaruzana kwenu, ingawa pia sio kwa kuruhusu mfanyakazi mwenzako akuandame bila sababu za msingi kwani pia itakuondoa kwenye mood ya kazi.

Jitahidi muda mwingi kuwa mtulivu sehemu ya kazi, chagua maneno ya kuongea kwa usahihi na fanya lolote kuondoa tofauti unazoona zinaweza kuleta mikwaruzano.

Na hata ikitokea pia jitahidi kutopenda kupendelea kukimbilia kushtaki kwa wakubwa zako wa kazi ingawa mwisho kama njia zote zikishindikana kuweka sawa tofauti zenu, basi ndipo itabidi kumuona kiongozi wenu asaidie kutatua.

4.Mavazi.
Kuna baadhi ya ofisi zinawataka wafanyakazi wake kuvaa sare(Uniform), aidha siku zote au kwa baadhi ya siku. Una bahati kama ofisi yenu haihitaji hilo, na kuwaruhusu kuvaa nguo yoyote unayojisikia.

Kama unatakiwa uvae uniform, hakikisha umevaa uniform muda wote kama inavyotakiwa.

Kumbuka kuwa kuvaa nguo za kubana au mguo fupi ni kujishushia heshima sehemu ya kazi.

Hata kama kabati lako lina nguo chache kiasi gani, hakikisha muda wote unaonekana msafi na nadhifu sehemu ya kazi.

5.Kujitenga.
 
Kama siku zote unataka kuwa mfanyakazi mwenye mafanikio sehemu yako ya kazi, basi jifunze mbinu za kufanya kazi pamoja na wafanyakazi wenzako na onyesha thamani yako mbele yao. Itakusaidia kuzalisha uhusiano mzuri na wao pamoja na mabosi zako.

Kama unataka kupunguza au kuepuka kabisa mawasiliano labda muda wa chakula cha mchana au muda tu uliowazi, basi jua unajiweka katika mazingira ya wenzako kusema,"huyu sio mwenzetu"!

6."Hiyo sio kazi yangu".
Kama inatokea mkubwa wako wa kazi anakuomba umsaidie kazi ambazo kiuhalisia sio sehemu ya majukumu yako ya kila siku, unaweza ukakubali au ukajibu "hiyo siyo kazi yangu".

Lakini kama una mawazo ya kuja kupandishwa cheo, kupendwa na wakubwa zako wa kazi au kupewa kipaumbele katika mambo mengi yenye manufaa, basi nyanyuka na saidia kazi hiyo badala ya kusema, "hiyo siyo kazi yangu."

No comments:

Post a Comment