LOGO

LOGO

Wednesday 14 May 2014

Tumfahamu Amber Rose!!

Anafahamika zaidi duniani kwa jina la Amber rose, lakini jina lake halisi la kuzaliwa nalo anaitwa Amber levonchuck huku akifahamika pia kama Amber Thot Rose.......

Amezaliwa huko nchini marekani, jimbo la philadelphia,pennsylvania, tarehe 21 Oktoba mwaka 1984.






Ana urefu wa futi 5 na inchi 8 au kwa lugha nyingine ana urefu wa mita 1.73. Rangi ya nywele ni zake ni Brunette (Dyed blonde wiyh buzz cut), huku macho yake ni ya rangi ya brown.

 
 
Akiwa na umri wa miaka 19, Amber rose ndipo alipoanza kujitebemea mwenyewe kimaisha kwa kuanza kufanya kazi ya kucheza uchi kwenye klabu za usiku huku klabu yake ya kwanza kufanya shughuli hizo za kucheza uchi ikijulikana kama kwa jila la Sue's rendezvous huko katika mji wa Vernon, westchester. 

 
Lakini jina lake lilianza kujulikana haswa baada ya kupata nafasi ya kutokea kwenye tangazo la Louis vitton akitangaza raba (Sneakers) za Lamon coleman. Na hapo ndipo milango ya umaarufu na mafanikio ilipofunguka rasmi. 


 Amefanikiwa kushiriki maonyesho mbalimbali ya mitindo kama New york fashion week akiwakilisha brand ya Celestino.Pia ameshiriki music videos mbalimbali za wanamuziki maarufu kama what them girls like wa Ludacriss, Vacation ya Young jeezy, massive attack ya Nick minaj, you be killing them wa Fabulous na no sleep ya wiz khalifa.

 
 
Ameshawahi kushiriki kwenye reality show ya Russel simmons, ameshashiriki NOH8 campaign, mwaka 2011 alikuwa jaji mwalikwa katika season 3 ya Ru paul's drag race na pia alikuwa jaji katika season 2 ya master of the mix kabla kuteuliwa kuwa msemaji wa kinywaji cha smirnoff na kutokea kwenye matangazo mbalimbali ya billboards na televisheni za matangazo ya kampuni hiyo akitangaza ladha mpya za kinywaji hicho za whiiped cream na fluffed marshmallow.

Amejaribu kuimba muziki pia kwa kutoa single yake ya kwanza 10 Januari 2012 aliyoipa jina Fame aliomshirikisha Wiz khalifa, iliyofuatiwa na single ya pili iliyoitwa loaded iliyotoka 06 Februari 2012. Pia amewahi kushirikishwa kwenye single ya 11 ya wiz khalifa iliyopo kwenye albamu ya O.N.I.F.C inayoitwa rise above pamoja na rapper Tiki carter na pharel williams ambaye ndio producer wa ngoma hiyo.

 
Ameshawahi kuwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper Kanye west kuanzia mwaka 2008 mpaka around mwezi wa nane mwaka 2010 walipotengana rasmi.

 
 
 
Mwanzoni mwa mwaka 2011 alianzisha uhusiano wa kimapenzi na rapper Wiz khalifa kabla kuvishana pete ya uchumba tarehe 01 Machi 2012 na kufunga ndoa rasmi tarehe 08 Julai 2013.


Amber rose na Wiz khalifa wamebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Sebastian Tylor Thomas aliyezaliwa tarehe 21 Februari 2013.

Rose na Khalifa wamekuwa wakigawa muda wao kwa kuishi katika nyumba zao mbili kati ya Los angeles na Cononsburg,pennsylvania.

 

Huyo ndio Amber Rose, mwanadada machachari, mrembo, mwenye mafanikio na swagger za hatari!!





No comments:

Post a Comment