LOGO

LOGO

Wednesday, 3 February 2016

Baaadhi ya Wanamichezo waliowahi kuonyesha kufuru ya matumizi ya pesa!

Mike Tyson.....
Huyu jamaa aliamua tu kununua Chui wawili ili aishi nao tu nyumbani. Ili mgharimu Tyson dola za kimarekani 140,000 kuwasafiriisha tu chui hao kufika nyumbani kwake na dola za kimarekani 4,000 kila mwwezi kuhakikikisha wanaangaliwa vizuri kila mwezi. Lakini pia vinyozi wa chui hao hawakuwa wa kuokota tu mitaani ilibidi kuwa wanaitwa proffessionals kuwanyoa na kuwaogesha tu. Kati ya vitu vinavyoaminika viilimfanya mkubwa Tyson afilisike......

Rickey Henderson.....
Huyu jamaa alipata umaarufu sana akiwa mcheza Mpira maarufu marekani wa base ball. Kikubwa kilichomfanya aingie kwenye list hii ni pale kwa mara ya kwanza alipopata cheki yenye pesa kubwa kabisa ambayo alikuwa hajawahi kuigusa katika maisha yake, Ni Cheki ya dola za kimarekani milioni moja,(USD ONE MILLION) Alichokifanya yeye aliichukua hiyo cheki, badala ya kwenda kutoa pesa benki, akaiframe tu, iwe kumbukumbu kwenye maisha yake! Ingawa ilibidi kumbukumbu yake hiyo ivunjike kwani waliompa deal hiyo team ya Oakland Athletics, walikuja kugundua kuna taatizo kwenye mfumo wao wa payroll kwamba kuna pesa haijatoka wakati walishaiandikia cheki so ili iweze kwenda sawa na masuala yao ya makato ya kodi ilibidi wamfuate jamaa na kumuambia akaitoe hiyo pesa. So kumbukumbu ikaishia hapo!


Novack Djokovic.
Huyu jamaa ni kati ya wana tennis bora kabisa duniani. Lakini tofauti na michezo, anafahamika kama mpenzi mkubwa wa kula cheese.

Kwa migahawa ya kawaida kupata cheese aina ya cheddar inaweza ikakugharimu labda dola 2 za kimarekani lakini huyu jamaa ananunua donkey cheese, chees iliyotengenezwa kwa nyama ya punda kwa kiasi cha dola 3,000 za kimarekani. Na aliwahi kununua donkey cheese yoote iliyokuwa tayari kuwa suplied dunia nzima yeye peke yake ili eti mtu mwingine popote duniani asile aina ya cheese atakayokula yeye!

Curt Schilling.
Baada ya kustaafu mchezo wa baseball, huyu bwana aliamua kuliweka jina lake hewani kwa kuannzisha video game studio aliyoiita 38 Studio. Sababu kuu ya kuiita video studio hiyo namba hiyo ni kwa kuwa ndio namba aliyokua akiivaa kwenye jezi yake wakati akicheza baseballl.

Alitumia dola za kimarekani milioni 50 kuifanya hiyo studio ianze kufanya kazi. Na ilifanyya kazi kwa miaka 6. Cha ajabu katika miaka 6 hiyo, ilifanikiwa kutoa game moja tu iliyoitwa Kingdoms off Amalur:Reckoning.

Inshort ilikuwa mbaya sana, kwa waliowahi kuicheza!

Allen iverson.
Huyu jamaa baada ya kuanza kupata pesa za kutosha alipoanza kucheza ligi ya kikapu ya NBA nchini Marekani, aliamua kitu kimoja , kila anaposafiri kucheza mechi alikua anaondoka na nguo aliyovaa tu. Nguo zote atakazovaa huko anapokwenda kwenye mechi basi ataenda kununua huko huko atakapofika.


Nelson Cruz.
Huyu jamaa ni mzaliwa wa Dominic republic. ambazo ni kati ya sehemu maskini kabisa duniani. Sasa jamaa yeye alichoamua baada ya kufanikiwa sana kwenye mpira wa baseball akaamua kwenda katika mji alioazaliwa huko kwao na kununua gari la fire, mji ambao kabla ya yeye kufanya hivyo haukuwa kuwa na gari hilo na hata gari la kubebea wagonjwa. So So good!!
 

Chriss Singleton.
Mcheza mpira wa kikapu! Alienda kucheza bahati nasibu ambayo angeweza kushinda dola za kimarekani 640,000. Ili ajiwekee mazingira rahisi ya kushinda,, aliamua kutumia dola  elfu 10 ambazo zilimfanya apate ticket za bahati nasibu 5000 ili apate hilo bunda. But...hakushinda!

Chad Johnson.
Alikuwa star wa American football.
Yeye aliamua kuweka a kweram(A fish tank) juu ya kitanda chake (A fish Tank as a headbboard). Sio mbaya na haicost kihivyo, but is it a real good investment?

Deshawn Stevenson.
Mcheza mpira ligi ya kikapu marekani,NBA, alichokifanya yeye ili kuondokana na vurugu za mabenki foleni na vitu kama hivyo, so akaomba ajengewe ATM machine sebuleni kwake ili aondokane na vurugu za  nje. I meann sebuleni kwake, sio mtaani kwake. Na gharama za kumjengea zilikua ndogo tu, dola za kimarekani 2,500 tu!
 

Vince Young.
Badala ya kukodi ndege binafsi tu kusafiria, huyu jamaa aliamua kununua siti za ndege nzima ya abiria ili asipande na mtu ndege nzima.  (Commercial flight). Wakati angekodi private jet, asingetumia kiasi kikubwa. Nafikiri masuala ya washauri tu, na ndio  maana si ajabu mcchezaji huyu wa Americann football alikuja kutangazwa kafilisika muda kadhaa baadaye..

Michael Beasley.
Jamaa yeye aliamua tu kumalizia pesa zake  kwenye Odd stuffs. Wenzake walikuwa wakimshangaa pesa zake zinatumikaje kwani muda wote alikuwa akinunua tu mapochi yaliyotumika, mito na vitu vya ajabu tu, ingawa inasemekana ni unga uliokuwa unampelekesha. Kweli inawezekana Star wa NBA ukapoteze fedha zako zote kwenye mapochi na mito iliyotumika?

Lenny Dykstra.
Ni mchezaji wa zamani wa baseball. Aliipenda sana nyumba ya mcheza hockey Wayne gretzky kiasi cha kuwaambia rafiki zake kwamba hajawahi kuona nyumba nzuri kama hiyo. Na kiukweli aliinunua kwa dola za kkimarekani 17.5 milioni ambayo ilikuwa ni kubwa kuliko thamani halisi ya nyumba.

Alipokuja kufilisika, wakati wa kufilisiwa kwake alijikuta akifungwa jela miezi sita  kwa kujaribu kujiibia vitu vya  ndani ya nyumba yake hiyo kwani ilikuwa tayari mikononi mwa bank. Self robbery!!!!

Arian forster.
Ukicheza American footblall na ukafanikiwa kuweka rekodi ya kukimbia 1,000 yards kwa miaka mitatu mfululizo then ni kitu kizuri.
Kuonyesha amefurahishwa na mchango wa wenzake, aliamua kuwanunulia scooters wenzake hasa wa upande wa offensive, 10 segway scooters ili wajumuike naye tu kwenye furaha.

Floyd mayweather.
Bondia.
Sina cha kumuelezea sana hopeful anafahamika dunia nzima kuanzia ulingoni mpaka  lifestyle yake.
Wakati wa superbowl kati ya Dennver Broncos na Seattle seahawaks, wengi waliamini Denver Brooncos watashinda akiwemo Floyd mayweather.

Katika kipigo walichopata Denver Broncos  cha 43-8 katika mechi hiyo ambacho ni historia katika Super bowl, Mayweather alikuwa ame-bet dola za kimarekani 10 milioni akiamini watashinda, so akaliwa kiasi hicho.

Ni kiasi ambacho hata kama bronchos wangeshinda, basi ni kiasi ambacho wasingekipata katika career yao kama wachezaji.

Patrick Peters.
Alipewa cheki ya  dola za kimarekani 15 milioni na timu yake ya Arizona cardinals ili asaini mkataba mpya . Hakwenda kuichuka hiiyo pesa benki, bali aliiweka tu hiyo cheki mezani jikoni kwake.

No comments:

Post a Comment