LOGO

LOGO

Thursday 11 February 2016

Mastaa waliojifungua watoto katika umri mdogo(Celebrities Got Birth when teenagers)

Kujifungua katika umri mdogo ni jambo ambalo si tamaduni nyingi duniani hufurahia, lakini pia si suala la tamaduni tu, bali hata kiafya wataalamu hawashauri uzazi katika umri mdogo. Lakini likishatokea ndio limetokea...hii ni orodha ya mastaa kadhaa duniani waliojifungua watoto wao wakiwa katika umri mdogo kabisa.


1.Maya Angelou.
Ni mwandika mashairi wa kimarekani ambaye yeye alipata ujauzito akiwa na umri wa miaka na kufanikiwa kujifungua mtoto wake wa  pekee aliyempa jina Guy Johnson.


2.Fantasia Barrino.
Ni mmarekani na Mshindi wa American Idol season ya 2004. Alikuwa nominee wa Grammy awards za mwaka 2014 katika categories 3. Mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 16, alijifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Zion Quari.


3.Roseanne Barr.
Alianza kama  mchekeshaji mdogo kwenye club ndogo ndogo mpaka mwaka 1985 akiwa na umri wa miaka 33 alipopewa nafasi kwenye kipindi cha The Tonight Show na pia kwenye kipindi cha Late Night With David Letterman mwaka uliofuatia yaani 1986. Kutokana na uwezo wake wa kuwafanya watu wacheke Roseanne Barr hatimaye alifanikiwa kupewa nafasi ya kufanya kipindi chake binafsi cha vichekesho kwenye studio za HBO, kipindi alichokipa jina "Roseanne".

Yeye alijifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na  miaka 17, amabaye alikuwa ni wa kike.


4.Loretta Lynn.
Anajulikana kama Qeen of Country music, akiwa ni mwanamuziki wa country music kuwahi kupewa tuzo nyingi zaidi duniani kwenye aina hiyo ya music. Aliolewa mwaka 1948 akiwa na umri wa miaka 15 tu na mwanaume aliyeitwa Oliver Doolittle, na kufanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza waliyempa jina Betty Sue akiwa na umri wa miaka 16, yaani mwaka mmoja tu baada ya kuolewa.


5.Solange Knowles.
American Singer,Songwriter, model na pia muigizaji Solange knowles, pia ni mdogo wa Beyonce. Yeye alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Daniel Julez J, akiwa na umri wa miaka 16.


6.Bristol Palin.
Mama yake ndio aliyempa umaarufu zaidi. Mama yake alichaguliwa kuwa Vice presidential candidate katika kipindi cha uchaguzi wa marekani mwaka 2008, uchaguzi uliowakutanisha John McCain na Barack Obama. Kutokana na shavu hilo la mama yake, moja kwa moja lilisababisha Media zianze pia kumfuatilia na yeye, hapo ndipo umaarufu wake ulipokuja, kwani akiwa na miaka 18 wakati mama yake yupo katikati ya Campaigns, Bristol Palin alijifungua mtoto wa kiume aliyepewa jina la Tripp Easton Mitchell.


7.Shirley Temple.
Shirley Temple aliwahi kushikilia rekodi ya mwigizaji mtoto kwenye miaka ya 1930's wakati akiwa ana miaka mitatu tu wakati alipoigiza kama nyota wa Movie ya Bright eyes.
Aliolewa mwaka 1945 na John Agar akiwa na umri wa miaka 17 na kufanikiwa kujifungua mtoto wa kike, Linda Susan, akiwa na umri wa miaka 19.


8.Sofia Vergara.
Sofia Vergara ni mzaliwa wa Colombia aliyehamia Marekani. Alianza masuala ya utangazi kwenye televisheni kwenye miaka ya  1990sS kwenye kituo cha Univision network kabla ya taratibu kujiingiza kwenye uigizaji kufikia miaka ya 2003's.
Amecheza movie kama Four Brothers na Hits mbili za Tyler perry ambazo nii Meet the Browns na Madea goes to Jail.
Alipata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 19.


9.Aretha Franklin.
Anatambulika kama The Qeen of Soul  ambaye alianza masuala ya music kama mwanamuziki wa nyimbo za gospel kwenye kanisa la baba yake. Alifanikiwa kuuteka muziki wa kidunia mwaka 1967 baada ya kufanya number one R&B hit single iliyoitwa I never loved a man(The Way I love You).
Alipata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 14 na kuongeza wa pili akiwa na miaka 15!!!


10.Anna Nicole Smith.
Alianza kufanya kazi katika mgahawa Fried Chicken mara tu baada ya kufukuzwa shule. Akiwa na miaka 18 aliolewa na Billy Wayne Smith na mwaka mmoja baadaye akiwa na miaka 19 walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume aliyeitwa Daniel Wayne.

Walitalikiana mwaka 1993, hakukata tamaa ya maisha kwa kujiingiza kwenye modelling na kufanikiwa kuwa Playboy playmate of the year mwaka huo huo wa 1993.


11.Niki Taylor.
Akiwa na miaka 13 ndio alianza rasmi kazi yake ya modelling. Na katika umri wa miaka 14, mzaliwa huyu wa Fort Lauderdale, Florida, nchini marekani alishinda shindano lake la kwanza la modelling na kuzawadiwa mkataba wenye thamani ya USD500,000. Akiwa at the early ages of 20's alifanikiwakupata watoto mapacha wa kiume, Jake na Hunter.


12.Keisha Castle-Hughes.
Mhamiaji huyu kutoka New Zealand kwenda Marekani, alipata bahati ya mtende baada ya kuchaguliwa kuwa muigizaji kiongozi  akiwa na umri wa miaka 13 tu kwenye filamu ya Whale Rider na pia kuwa kuwa the youngest ever actress kuchaguliwa kugombea tuzo ya Academy awards kwa muigizaji bora wa kike.
Akiwa na umri wa miaka 16 tu yeye na booyfriend wake Bradley Hull walitangaza ujauzito na kupata mtoto wa kike aliyeitwa Felicity Amore Hull.


13.Savannah Brinson.
Lebron James ni mchezaji  mkubwa wa mpira wa kikappu nchini marekani alichaguliwa first overall pick kwenye draft za NBA mwaka 2003 moja kwa moja toka  high school, na kipindi hicho shuleni hapo alikuwa ana mpenzi aliyeitwa Savannah Brinson. Kitendo cha yeye kuchaguliwa kuingia NBA kilipaisha vilivyo jina la Savannah Brinson kwani kila akipita sehemu utasikia yule ni mpenzi wa Lebron James.
Walifanikiwa kupata mtoto wakati Savannah Brinson akiwa na umri wa miaka 18, mtoto wa kiume, aliyepewa jina la LeBron,Jr.


14.Naomi Judd.
Mwanamuziki wa Country music ambaye hapo awali hakuwahi kufikiria kabisa kuwa mwanamuziki kwani alisomea nursing. Alipata mtoto wake wa kwwanza wa kike, Christina Ciminella, akiwa na umri wa miaka 18.


15.Jamie Lynn Spears.
Ni mdogo wa mwanamuziki Britney Spear. Yeye zaidi ni muigizaji aliyefanikiwa zaidi baada ya kuanzisha network serious yake iitwayyo "Zoey 101". Akiwa na umri wa miaka 16 alitangaza kuwa ni mjamzito na kuja kujifungua mtoto wa kike, aliyepewa jina, Maddie.


16.Emily Maynard.
Ni muigizaji aliyejipatia umaarufu kupitia reality show ya The Bachelor and The Bachelorette inayoonyeshwa kwenye Televisheni ya ABC. Mchumba wake aliyekuwa akiitwaa Ricky Hendrick, ambaye alikuwa ni dereva wa magari ya mashindano yaendayo kasi, NASCAR, mwaka 2004 alifariki baada ya kupata ajali akiwa kwenye mashindano. Muda mfupi tu baada ya kifo hicho ndipo Emily Maynard alipogundua kuwa kumbe alikuwa na ujauzito wa mchumba wake huyo, na alijifungua mtoto  aliyempa jina Josephine Hendrick, yeye akiwa na umri wa miaka 19.

No comments:

Post a Comment