LOGO

LOGO

Thursday 4 February 2016

Celebrities Waliowahi kubadili jinsia!!

Kuna watu sijui hawapendi kujiona walivyoumbwa, au sijui utandawazi, au sijui ndio wanasema homoni. Mtu anazaliwa dume anaamua kujibadilisha kuwa mwanamke. Mwanamke anazaliwa anaamua kujibadilisha kuwa  mwanaume. Anyway kila mtu na maamuzi yake, tuwaone baadhi yao.

Bruce Jenner....
Alizaliwa dume akijulikana kama Bruce Jenner baadaye akaamua kujibadilisha jinsia na kuwa mwanamke na kubadili na jina pia kuwa Caitlyn Jenner.


 Laverne Cox.
Anajulikana Zaidi baada ya kushiriki kwenye Netflix show orange in the new black, lakini pia alikuwa mtu wa kwanza kubadili jinsia na kuchaguliwa kwenye Primetime Emmy awards.


Janeth Mock.
Former People staff editor Janeth Mock alikuwa mwanamke rasmi alipofikisha umri wa miaka 18. Lilikuwa Dume!!

Andreja pejic.
Alikuwa  ni supermodel wa kiume lakini akionyesha mavazi yote, yaani ya kike na kiume kabla ya mwaka 2014 kuamua kujibadilisha jinsia na kuwa binti!!


Caroline cossey
British actress ambaye pia aliwahi kufanya kazi pia na Playboy na aliwahi kuonekana katika movie kama Bond girl kwenye movie ya For your eyes only.


Jenna Talackova.
Mwaka 2012 alipigania kisheria na kufanikiwa kuruhusiwa kushiriki Miss universe Canada kwani mwanzo alikataliwa kwa kuwa alikuwa amebadilisha jinsia kutoka uanaume na kuwa mwanamke. Anywahi alifanikiwa kushinda kipengele cha Miss Congeniality!




Alexis Arquette.
Alizaliwa mwanaume kwa jina la Robert kutoka katika familia maarufu katika uigizaji ya Arquette, kabla ya kujibadilisha jinsia na kujipa jina la Alexis.


Isis King.
Aliwahi kuwa  mshiriki wa 11th cycle na 17th cycle ya reality television show ya America's next top model.

Chaz Bono.
Mtoto pekee wa wazazi Sonny na Cher. Alizaliwa mwanamke akijulikana kama Chastity, lakini alikuja  kubadili jinsia kutoka mwanamke kuwa mwanaume na kujipa jina Chaz.


Sylivia rivera
Mmoja wa mwanachama mwanzilishi wa Gay liberation front na The gay activists alliance na pia mmoja wa waanzilishi wa Street transvestive action revolutionaries, kikundi kinachosaidia vijana wa mitaani.



Christine Jorgensen.
Aliizaliwa kama George William Jr, na huwezi kuamini alikuwa ni askari aliyekwenda kupigana vita vya pili vya dunia akiwa na jeshi la marekani kabla ya kubadili jinsia baada ya kumaliza  utumishi wake jeshini.

Candy Darling.
Alizaliwa kwa jina la James Lawrence slattery. Aliwahi kuonekana katika movie ya Andy Warhol's iliyojulikana kama Flesh na pia katika  movie ya Women in Revolt.


Carmen Carrera.
Ni model aliyewahi kufanya pia movie kama RuPaul's Drag race na Real housewives of new York city na alitangaza kupitia television kuwa amebadili jinsia kutoka mwanaume na kuwa mwanamke.



Ian Harvie.
Ni Comedian, aliyezaliwa kwa jina la Janet kabla ya kujitokeza hadharani akiwa na umri wa miaka 32 kujitangaza hadharani  kuwa amebadili jinsia kutoka mwanamke na kuwa mwanaume.

Lana Wachowski.
Kati ya Maproducer bora kabisa duniani ambaye aliwahi kushiriki kutengeneza movie za Matrix, V for vendetta, speed racer na Cloud Atlas.



Lea T.
Alizaliwa mwanaume akijulikana kama Leandro kabla  ya kubadili jinsia na kujipa jina Lea.

Raffi Freedman - Gurs pan.
Pamoja na kujibadilisha kwake kutoka mwanaume kuwa mwanamke hilo halikuziba nyota yake kwani mwaka 2015 alipata zali baada ya kuteuliwa na Raisi Obama kuwa kama Outreach and recruitment director.



Nadia almada.
Ni British reality show star, aliyezaliwa mwanaume kwa jina la Jorge leodoro na pia kuwa mtu wa kwanza aliyebadili jinsia na kushinda Big brother series 5 ya mwaka 2004.

Coccienelle.
Alizaliwa mwanaume akijulikana kama Jacques Charles dufresnoy kabla ya kubadili jinsia na kujipa jina la Coccienelle.


Ballian Buschbaum.
Mshiriki wa zamani wa Olyimpic akipeperusha  bendera ya Germany. Aliacha rasmi mambo ya michezo mwaka 2007 na moja kwa moja akaenda kubadili jinsia kutoka mwanamke na kuwa mwanaume.



No comments:

Post a Comment