LOGO

LOGO

Thursday 11 February 2016

Usafiri wa ndege unapogeuka kero, badala ya Luxury!!

Tunaamini usafiri wa ndege ni usafiri salama, wa haraka na kikubwa zaidi ni Luxury, yaani unasafiri ukiwa unaenjoy na ukiwa umerelax. Lakini unaweza siku ukapanda ndege ukakutana na mambo yatakayoweza kukufanya uone safari yako ni ya kuchosha kabisa. Hebu tuone baadhi ya mambo....

1.Jamaa hajali kabisa kuhusu mtu aliyekaa nyuma yake, kwa kuamua kulaza kiti hivyo kuchukua nafasi ya mtu wa nyuma yake. Huwezi kufurahia hali hii safarini....

2.Kuna tabia kama ya kupiga mateke  viti kwa nyuma, so kama wewe umekaa mbele yao basi ni kama watakuwa wanakutandika wewe mateke ya mgongo. Halafu hapo utakuta kakaa na mzazi, lakini wala hakatazwi.

3.Pale Seats za ndege zinapokuwa ndogo, halafu ukapangiwa mtu mnene. Hata kama akijaribu aenee kwenye seat yake, bado usumbufu utakuwepo.

4.Watoto wanakaribishwa kwenye ndege, lakini pale wanapoanza mambo yao ya kuimba kwa sauti ya juu huku wakisaidiwa kwa nguvu na midoli yao inayotoa sauti mbalimbali, hapo ndipo utakapoona safari ni chungu. Na kikubwa zaidi watoto hao sio wako, ni wa abiria mwingine!!

5.Pale unapopangiwa seat ya katikati, kwenye seats tatu halafu abiria wa kushoto kwako anataka kumuongelesha kila wakati abiria wa kulia kwako. Au hata abiria wa nyuma yako, au pembeni yako anapojaribu kujizungusha huku na kule kuongea na abiria ambaye hawajakaa pamoja.... Inaboa!!

6.Kuna wale, wanaoingia ndani ya ndege wakiwa na mabegi makubwa ajabu, wala hajiulizi kabla hajapanda kuwa yatafit katika sehemu maalumu za kuwekea mizigo au la, yeye anapanda nalo tu. Inaleta  usumbufu sana.

7.Unataka kuangalia Movie? Huyu jamaa anaamua kusimama na kuamua tu kwamba hakuna atakayeona movie hiyo. Si ukae chini jamani!!

8.Kuna wale wanaopenda kusimama mara kwa mara. Mara kanyanyuka kuchukua kitu kwenye begi, mara kanyanyuka tena kukirudisha. Mara kanyanyuka anakwenda chooni, sekunde kadhaa ananyanyuka kwenda kumuongelesha nani sijui, si utulieee.....

No comments:

Post a Comment