LOGO

LOGO

Thursday 11 February 2016

Jennifer Lawrence Naye kwenye mambo ya Red Carpet, pamoja na historia yake fupi.

Jina Lake kamili anaitwa Jennifer Shrader Lawrence, ni muigizaji wa kimarekani aliyezaliwa tarehe 15 August, 1990 huko Loisville,Kentucky, nchini marekani.
 

 
Mama yake anaita Karen aliyezaliwa mwaka 1956 na baba yake ni Gary Lawrence. Ana kaka zake wakubwa wawili ambao ni Ben na Blaine. Alisoma katika shule ya Kammerer Middle school huko Loisville.
 
 
 
Alianza kuonekana awali kabisa akiigiza kama kiongozi  kwenye TBS comedy series iliyoitwa The Bill Engvall Show kati ya miaka ya 2007 -2009, na pia alikuja kuonekana kwenye drama iliyotoka mwaka 2010 iliyoitwa Winter's Bone. Lakini mafanikio yake hasa kibiashara ni pale alipocheza filamu ya X-Men:First class, mwaka 2011.
 
 
 
Amecheza pia kwenye series ya Hunger game, mwaka 2012-2015, ameonekana pia kwenye Romantic comedy iitwayo Silver linings playbook iliyotoka mwaka 2012, ambayo ilimfanya kufanikiwa kupata tuzo kadhaa kama Golden Globe award, a screen actors Guild Award na Academy award kama muigizaji bora wa kike, tuzo iliyomfanya kuwa mwigizaji bora wa kike wa pili kijana Zaidi kuwahi kutwaa Best Actress Oscar Winner. Na pia baada ya kucheza katika Drama ya American Hustle iliyotoka mwaka 2013, alifanikiwa kushinda tuzo za BAFTA Award na Golden Globe Award.
 
 
Baadhi ya movie nyingine alizocheza ni, Garden Party, The Poker House, The burning plain, Like Crazy, The Beaver, House at the end of the street, The devil you Know, Serena, Joy na nyinginezo.
 
 
 

Kwa upande wa masuala ya kujitolea katika jamii hayupo nyuma. Yupo na World food programme, Feeding America na First Project. Aliwahi kuorganize early screening ya  movie The hunger games:catching fire kwa ajili ya kuchangia Saint Mary's center, kituo maalumu cha kuhudumia wenye ulemavu kilichopo mji aliozaliwa, na alifanikisha kupatikana kiasa cha USD 40,000 kwa ajili ya kituo hicho.
 
 
Pia yeye ni official ambassador wa special Olympics, organization kubwa ya michezo duniani inayojihusisha na mashindano ya michezo ya watoto na wazee wenye ulemavu mbalimbali. Pia ana Jennifer Lawrence Foundation inayosaidia miffuko mbalimbali kama Screen Actors Guild foundation, Special Olympics na Do something, shirika linalojishughulisha kuwaamsha vijana kuchukua hatua katika mabadiliko ya kijamii yanayowazunguka. Hayo ni baadhi tu kwa ufupi kumuhusu Jennifer Lawrence.  

No comments:

Post a Comment